Nikasababisha kifo cha mke wangu kwa sababu ya penzi la kahaba………….!

Dahhh!bonge la darasa aisee!so huko ukweni unawakumbuka na kuwapa msaada wowote?na vp ulishaoa mke mwingine?na mkeo unamuenzi vp?kama wewe ni islamic tubu kwa mola wako kisha jenga japo "madrasa"then ipe jina la mkeo kisha ikabidhi kwa waislam ili waitumie ktk kupata elimu.
 
...unajuta nini wakati iliwahi kusemwa " usimnyanyase mke wa ujana wako"
 
Kwenye thread kama hii kwa sababu mbaya ni mwanaume utasikia "wanaume wabaya sana", "wanaume acheni mahawara".Ikija story ya mwanamke nao wataonekana wabaya sana.

Kumbe katika jinsia zote kuna makatili
 
Hakuna hawara ambaye ameshawahi kuleta mafanikio. Acheni wachune hadi tubaki mbavu na siku hizi ni ukimwi tu. Ni fundisho pia kwa wale tunaothamini hawara kuliko mke aliyekuwezesha kupata mali na utajiri mwingine na hela then siku mmoja unambatiza mbwa, takataka, shenzi, huna adabu, n.k But malipo hapa hapa duniani.
 

Ulianza
 
what goes around comes around...........................pole sana
 
Ulianza vizuri Bongo movie yako, then hapo katikati ukayakoroga. Anyway, movie yako inatoa mafunzo mazuri ktk jamii.
 

Vulgar!
 
Cha ajabu trend ni ile ile na hatujifunzi?
Mdingi, inabidi tukupeleke ukacheki na hiv, nna wasiwasi!
 
Lol Mtambuzi wewe umepitia visa na mikasa mingi! Nakumbuka kisa cha ndoa yako ya
mkeka kule Ununio!! Halafu pia ulifanikiwa kutimka na kumwacha mkeo. Au ndio ilikuwa laana/mkosi
wa kile kibinti ulichokiacha?
 
Last edited by a moderator:
Wewe utakuwa huna adabu kabisa na moyo wako utateseka hadi kufa. **** mkubwa.
 
Lol Mtambuzi wewe umepitia visa na mikasa mingi! Nakumbuka kisa cha ndoa yako ya
mkeka kule Ununio!! Halafu pia ulifanikiwa kutimka na kumwacha mkeo. Au ndio ilikuwa laana/mkosi
wa kile kibinti ulichokiacha?

Mkuu huu mkasa ni wa kweli lakini haunihusu mimi, kuna mdau aliusimulia na mimi nimeona ni vyema niweke hapa ili watu wapate kujifunza
 
Cha ajabu trend ni ile ile na hatujifunzi?
Mdingi, inabidi tukupeleke ukacheki na hiv, nna wasiwasi!

Mwanangu huu mkasa ni wa kweli na unamuhusu msomaji wa Gazeti la Jitambue, niliwahi kuuandika katika gazeti hilo miaka sita iliyopita.......................Wakati huo mtoa ushuhuda akiwa na miaka 40.
Mkasa huu sio miongoni mwa vile visa vyangu vya UNUNIO............LOL
 
Ntambuzi story ya leo kali hasa ulipomtumia huyo dada wa kichagga nimecheka sana, yaani anafilisi duka na kuwaingiza kaka zake ndani. Story ninpale uliposema ww ni dereva halafu ukabaki na hawara kwa nini usisafiri naye au kumpangia chumba.
hata hivyo safi sana na nakuogopa kwa uchambuzi wako wa Hekima usisahau na kesi kubwa kubwa za mahakamani wiki hili tumwagie
 
Story nzuri...lakini duuuh ndefu sana. Kwa mimi hapa ninaona mambo matatu



-Wanawake wa kichaga matapeli wa mapenzi na wafilisi

-Wanaume wa kileo hawaheshimu ndoa zao hata kama mmeanza mbali akipata mjuzi zaidi huna chako.

-Wanawake wajinga, wanataka elimu zaidi ili wajikomboe. Huyo dada wa Turiani aliyejiua kwa sababu ya aibu ni aibu gani hiyo. Hizo ndio challenges za wanawake zinazowakuta, mambo ya kuogopa jamii itawaweka katika category gani.
 
I see kumbe mtambuzi ulikuwa unaandikia jitambue?aisee ndo mana,kwanza shikamoo.umenikumbusha nikiwa Primaryto O level hilo gazeti nilikuwa nahakikisha hailinipiti nakumbuka lilikuwa linatoka jumanne cjui na cku gani baadae likapoteaga nikasikitika kweli manake huwa sinaga mazoea ya kunua magei mengine.ukweli hata hapa napenda kusoma unachoandika najifunza mengi sanna hongera kama sio babu basi baba manake jitambue nimesoma nikiwa naanza kufunguka macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…