Nikasome ipi kati ya masters ya education au nitafute bachelor ya kitu kingine

Nikasome ipi kati ya masters ya education au nitafute bachelor ya kitu kingine

Darwin Nunez

Member
Joined
Jun 12, 2022
Posts
90
Reaction score
212
Habari wanajamii

Nimekuwa katika wakati mgumu baada kumaliza masomo yangu level ya bachelor degree tangu mwaka 2015 kwani sijawahi pata ajira yoyote ile

Kwa sasa nina miaka 32, nauona uzee huu hapa unasogea ikiwa sina mali, mke wala kitu cha thamani ninachomiliki na mbaya zaidi naishi nyumbani though nilitimuliwa nikarudi tena

Sasa familia imeamua kunipa nafasi ya pili nichague kipi nikasomee either nikaendelee na masters ya ducation masomo ya sanaa au nitafute degree nyingine niisome nikimaliza nitafute kazi

Naombeni ushauri
 
Habari wanajamii

Nimekuwa katika wakati mgumu baada kumaliza masomo yangu level ya bachelor degree tangu mwaka 2015 kwani sijawahi pata ajira yoyote ile

Kwa sasa ninamiaka 32, nauona uzee huu hapa unasogea ikiwa sina mali, mke wala kitu cha thamani ninachomiliki na mbaya zaidi naishi nyumbani though nilitimuliwa nikarudi tena

Hiyo ada ya kutosha kusoma masters degree kwanini usifanyie biashara?
 
Kwani wewe huwezi fanya biashara huwezi fanya uwekezaji mdogo mdogo hiyo gharama ya kusoma ungekuwa na akili timamu ungeshawekeza kwenye kitu ambacho kesho na siku zijazo kitakusaidia. Ni hatari sana kama una 32 na huna kipato cha uhakika lini utakuwwa na asset zako uliowaacha mtaani wamekupita kwa uwezo uliowaacha shule ya msingi wakaendelea na maisha ya mtaani saa hizi wana familia na kipato endelevu.

Sawa home wanataka usome ila waoneshe kuwa una njia nyingine unataka kupita waonyeshe malengo yako future yako (ila kama unayo) ni aibu 32 kuwa home na huna chochote angalau ungekuwa 32 halafu unasimamia miradi na kuendeleza biashara za home sawa ila huna kitu alooo shame on you unatuaibisha vijana wachapa kazi.

Na familia yako hawajakulea kujua mazingira ya dunia ya sasa yanahitaji nini.
 
Habari wanajamii

Nimekuwa katika wakati mgumu baada kumaliza masomo yangu level ya bachelor degree tangu mwaka 2015 kwani sijawahi pata ajira yoyote ile

Kwa sasa ninamiaka 32, nauona uzee huu hapa unasogea ikiwa sina mali, mke wala kitu cha thamani ninachomiliki na mbaya zaidi naishi nyumbani though nilitimuliwa nikarudi tena

Sasa familia imeamua kunipa nafasi ya pili nichague kipi nikasomee either nikaendelee na masters ya ducation masomo ya sanaa au nitafute degree nyingine niisome nikimaliza nitafute kazi

Naombeni ushauri
Chukua Hela nunua hata bajaji, ukae mwenyewe undeshe, kwenye shule nowadays ni bet Hatari...
 
Nishapewa mtaji mara kadhaa nikadunda
Biashara sio ya kila mtu
kwahyo unatarajia kuajiriwa bas kaa ukijua ajira pia sio ya kila mtu kama umesota 5yrs huna ajira unaeza ukafa hujaajiriwa huna mtt wala huna kitanda. kwenye maisha yangu sijawahi na sitokaa kuwa na msela apewe mtaji ashindwe kuuendeeza inamaana tatizo lipo kuanzia home company yako wale wanaokuzunguka na ww mwenyewe kichwa chako na machaguzi ya maishagani uishi
 
Kama ulisoma Bachelor of Education, ukitaka uzidi kupoteza muda na ujiongezee stress za maisha basi nenda kasome Masters ya aina yoyote ile.

Ila kama ulisoma Bachelor degree ya fani tofaut na Education, nakushauri kasome Postgraduate ya education kwasabab itakuongezea possibilities ya kupata nafasi ya kuajiriwa kuwa Mwalimu.

Ukae ukijua serikal hawamuajiri mtu kwasabab ana Masters, serikali haimuongezi mfanyakaz cheo au mishahara kwasabab ana Masters.

All in all hiyo ada ya masters ni heri ufungue biashara ujaribu bahat yako...
 
Pole sana kiongozi, nadhani ungejaribu kujibiidisha kwenye kilimo maana bado utakuwa unapoteza pesa, Master unaweza tumia million 5 na ni kiasi kikubwa

Sent from my CLT-L29 using JamiiForums mobile app
 
Hao wanataka ukasome km njia ya kukutimua home,unaweza kuomba pesa ufanyie biashara wakagoma ili usiendelee kurud home,ko we play smart chukua iyo ada ya miaka mi3 potelezea dunian mazma kalime
 
Swala la kufanikiwa linaanza na wewe binafsi na wala sio influence ya mtu mwingine yeyote.

Tangu uwe graduate mpaka sasa ni miaka 7.

Ungeamua kujishughulisha na vibiashara vidogo vidogo now ungekuwa upo mbali.

kama ulikosa ajira kupitia iyo professional yako,Je unafikiri ukisoma bachelor ya education au masters ndio upepo utabadilika.?

Si kila mtu ameandikiwa atatoboa kupitia kuajiriwa,Try biashara huenda utatoboa.
 
Kama ulisoma Bachelor of Education, ukitaka uzidi kupoteza muda na ujiongezee stress za maisha basi nenda kasome Masters ya aina yoyote ile.

Ila kama ulisoma Bachelor degree ya fani tofaut na Education, nakushauri kasome Postgraduate ya education kwasabab itakuongezea possibilities ya kupata nafasi ya kuajiriwa kuwa Mwalimu.

Ukae ukijua serikal hawamuajiri mtu kwasabab ana Masters, serikali haimuongezi mfanyakaz cheo au mishahara kwasabab ana Masters.

All in all hiyo ada ya masters ni heri ufungue biashara ujaribu bahat yako...
Nashauri azingatie yote uliyomwambia isipokuwa la kwamba kama amesomea fani nyingine tofauti na uwalimu akasome postgraduate ya ualimu ili aje aajiriwe, hilo haiwezekani siku hizi hawaajiri walimu wa aina hiyo
 
Nishapewa mtaji mara kadhaa nikadunda
Biashara sio ya kila mtu
Sikushauri kufanya Masters kwa sasa maana kama hujafanyia kazi ulichosomea ngazi ya bachelor degree si rahisi kupata kazi ukiwa fresh masters labda kama utapata zali la kufundisha chuo na hii ni endapo ulipata GPA nzuri undergraduate.

Pili kusomea degree nyingine umejihakikishia ndo itakua na ajira? Unless otherwise uende ukasomee fani itayokufanya ujiajiri.
 
Back
Top Bottom