philosophy
Senior Member
- Nov 11, 2012
- 104
- 42
NI KILE MIMI NINACHOKIKUBALI NA KUKUAMINI KAMA NJIA YA MAENDELEO KWA BINADAMU
Siku zote huwa nina msimamo thabiti kuhusu uhalisia na ukweli juu ya kuendelea kwa binadamu. Kwangu mimi si mali au utajiri wowote ya kwamba ndio kuendelea kwa mtu; bali nitahubiri zaidi katika fikara/fikra za binadamu ambazo chanzo chake ni urazini /akili ambayo ndio ukiini wa mwanadamu tofauti na wanyama wengine. Akili ndio maendeleo kwa mtu yeyeote yule hasa pale anapotambua na kutumia upekee huo. Hivyo, kila kilichopo kwa uwezo wa binadamu hakika hakiwezi kumzidi nguvu au thamani hata kama kinahusudiwa kuliko.
Katika udhihirisho huo wa ukuu wa mwanadamu na thamani yake ulimwenguni, hakika kufikiri hakuhepukiki kwani kufikiri na kutafakari ndiko kunakompa mtu kutambua hiki na kile au kumpeleka katika ugunduzi hatimaye kuwa mwanadamu bora na kuyafurahia maisha yake. Kinyume chake ni shida tupu zaidi ya kuwa mtumwa wa maumbile yake. Kumbe haya sikuyafikiria mimi pekee, bali hata baadhi ya watu wengine wakiwemo wataalau kama mtaalamu wa falsafa hapa nchini Dr. Adolf Mihanjo, katika kitabu chake Falsafa na Ufunuo wa Maarifa, aliliona hili kwa kusema haya yafuatayo, namnukuu:
[Mahali popote pale ambapo binadamu mwenye akili timamu anaishi na siyo mfu hapakosi mpambano ya . mapambano ya hoja ndio hali halisi ya uishi wa binadamu katika mazingira ya mapungufu yake. Hivyo, mathalani binadamu anaishi na kufikiri, anakuwa na maswali mengi nadani ya kina cha roho yake , kuwa, hivi haya ninayoyaamini kuwa ni ya kweli, kweli ni ya kweli? Naweza kuyathibitisha vipi ukweli wake? Au haya maisha ninayoishi ndio maisha ambayo yanipasa kuishi? Hakuna namna nyingine ya kuweza kuyaeleza haya ninayoyaamini kuwa ni ya kweli, kweli ni ya kweli?]
Katika ukuu wake mwanadamu, hakika kufikiri kwake kutakuwa sehemu kubwa ya maisha yake kwa sababu yeye anayaishi na kutafakari mazingira na maisha yake. Hivyo, dhana mbalimbali ataziibua na kuzielezea kwa kuweka misingi ya hoja zake. Na kwa kuwa wakati anafikiri na wenzake pia wamo katika harakati hizo kwa kuwa sio wafu, basi nao wataziibua dhana zao kwa hoja zao na hivyo kuibuka mvuvumko wa malumbano au mapambano ya hoja katika mlolongo huo, ugunduzi na utafiti wa aina tofauti huwa ni zao la akili ya binadamu. Na hivyo kile tunachokiita maendeleo kuibuka.
Kumbe basi, wewe au mimi, sote tutakuwa tu wafu kama sio wapuuzi kuukataa ukweli wa mapambano ya hoja. Ndugu mtanzania mwenzangu, tujaribu kuzama katika dimbwi hili la kufikiri kwa dhana ngumu na hoja ngumu ili yaibuke malumbano/mapambao ya hoja kwa mustakabali wa taifa letu na maendeleo kwa ujumla.