Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
.......Nikifanikiwa kuzeeka
Nitawaambia wanangu nitakaojaaliwa, wasifikiri nilicheza kwa kuwa hawajapata urithi wa maana. Niliwahangaikia sana, lakini jitihada haikushinda kudra. Nitawaeleza waishi vizuri na watu, Ili wasije kupata tabu.
Nitawasisitizia kuwekeza japo kidogo, kwa kuwa hawajui kesho yao. Nitawaambia kuwa penda utakavyopenda ila Kuna siku utaachwa katika mstari uliopinda sana na hutoamini, lakini ndio maisha wajiandae kupambana.
Nitawaeleza pia kuhusu wanawake na vitimbi vyao na jinsi ya kuishi nao. Sitosahau kuwaambia kuhusu Mungu wao, na jinsi anavyoweza kuwaokoa walipokata tamaa.
Lakini mwishoni nitawakumbusha, washirikiane kadri wawezavyo ila wasisahau kuwa Mwisho wa Ushirika ni kugawana, wajiandae kwa Hilo
Maringo