Hii kitu mkuu bado haijakaa vizuri kabisa kwa upande wetu sisi wakazi wa Kigamboni,ila watu wanajenga kwani mpango haujakuwa wazi na hao watendaji wenyewe hawako wazi kama inavyo paswa na ilivyo elezwa na wachangiaji hapa.
Ni hivi karibuni tu,waziri mwenye dhamana ya ardhi MH. Mama,Pfs.Tibaijuka kwenye mkutano wa hadhara pale Machava alisema wazi wazi kwamba "MTAHAMA",pamoja na maswali mengi juu ya hilo la kuhama hakujibu swala la msingi, "...ni vipi tutahama..??" ikiwa na maana ya thamani,malipo na wapi tutapelekwa kama fidia inavyo elekeza kwenye mpango kazi wa NEW CITY.Watu walimuuliza maswali mengi lakini hakujiibu kitu zaidi ya MTAHAMA.
Lakini muda unakwenda na hakuna lolote la maana lilokwisha fanyika kwa upande wa serikali/muwekezaji/wawekezaji zaidi ya ile ASSESSMENT iliyofanyika miaka miwili iliyopita yaani 2009 baada ya hapo ni kimya zaidi ya habari iliyotolewa kwenye gazeti la mwana nchi la Aprili na siku zisizo zidi wiki kufatiwa na Mkutano wa Mama Tibaijuka.
Sasa,kama mmiliki na mwananchi/binadamu muda hausimami kwako toka bandiko la MARUFUKU kuisha muda wake na hari za ugumu wa maisha kupanda kwa maana ya kodi za nyumba na vifaa vya ujenzi,......"ushauri wangu"......"kama ulikua una ramani tayari ya ujenzi,basi jenga hata servant quarter/vyumba viwili au vitatu na choo kwa rugha ya Darsalam Banda la uwani kupunguza makali hayo ya maisha kwani ardhi unayo na haina faida kukaa buree wakat hata bank hauwezi kuitumia kukopa (ila kwa mshangao wangu recently ACCESS BANK wanaweza kukukopesha ukiwa na jengo zuri na hati/offer,si jui kwa ma-BANK mengine kama wameshaanza TENA kukopesha).
,shida hizi za ukali wa maisha watendaji wetu wamezifumbia macho,ukiwa na kibdanda chako Kigamboni,kama sio mbali sana hata kwa miguu mjini unafika kupunguza NAURI za daladala na Misongamano ya foleni zinazo zidii mjini (ingawa sasa hata huku pia foleni za magari kuvuka kivuko zimeongezeka,kutokana na uzembe wa waendesha hivyo vivuko,mabaharia na menejimenti kwa ujumla wao) ni bola kuweka jengo la bei rahisi ambalo ikiwa utavunjiwa basi iwe sawa na KODI YA MIAKA MIWILI AU MITATU kwa nyumba ya kupanga mjini!....narudia tena huu ni ushauri wangu