Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Wakuu. Hii SGR imeanza kwa mbwembwe nyingi kama zilivyoanza kampuni nilizozitaja hapo juu zikisimamiwa na serikali kama DART ambayo ilianza kwa mbwembwe nyingi kama SGR ikuwa na mabasi ya kisasa yenye kamera, screen, mike zikifanya kazi na mpangilio mzuri wa tiketi hadi kutumia kadi na simu. Leo kiko wapi hata miaka 15 haiijafika mabasi na huduma choka mbaya afadhali hata ma DCM ya Mbagala.
Ninachotaka kusema kwa ufupi serikali hata siku moja haijawahi kusimamia biashara ikafanikiwa. Hivyo wenye mabasi imarisheni huduma wala hamtakosa biashara kwakuwa kama ingekuwa hivyo TAZARA na TRC ya kati zingewaondoa barabarani lakini zipo ICU. Kauli ya kuwa eti wenye mabasi kama Abood wajiandae kutafuta rotes nyingine si ya kutiliwa maanani ni suala la muda mfupi sana na tayari tumeshaona maneno na mayendo yao ni tofauti tren imezima usiku zaidi ya saa 2 wakati walisema itakuwa na back up. Tatizo ni kuwa hakuna uzalendo katika kuendesha taasisi za umma na watu kupeana vyeo na nafasi kwa connections badala ya uwezo. Taasisi zote ambazo wafanyakazi wake wanaajiriwa kwa mtindo wa ajira ya kudumu na kuteuliwa huwa hazina ufanisi kwakuwa mtu wa kuteuliwa anakuwa hana uhakika kama kesho atakuwa hapo hivyo huona ni bora achukue chake mapema. Wa kudumu asiye na mkataba anakuwa na kiburi kwakuwa anajua hafukuzwi kazi mpaka astaafu.
Kiufupi ni kuwa serikali haiwezi kuendesha biashara yenyewe inatakiwa ikusanye kodi na kupeleka maendeleo kwa wananchi. Tunzeni andiko hili zikianza segemnege mtakumbuka maana hata DART JPM aliizindua kwa mbwembwe nyingi kwa kupiga mahoni kibao leo iko wapi?
Siiombei mabaya SGR lakini sina imani nayo kabisa. Kama tulishindwa TAZARA, RELI YA KATI, KAMATA, UDA, ATC na makampuni ya mikoa leo reri compicated kama ya umeme tutaiweza wapi? Tumeshaona hata mwezi haujaisha ngedere ambaye hatembei usiku anakuwa kalala zake kwenye mapango na miti kapewa kesi ya kukata umeme wa SGR. Kama mtu alikuwa na akili angembambikia kesi hii komba. Bundi naye kabambikiwa kwasababu ya ushahidi wa kimazingira kwamba yeye huruka usiku. Who knows? Kesho tusishangae kuambiwa ni nyoka au panya