Pole sana.Hizo ni dalili za Gastritis kitaam.Kwa lugha yab kawaida ni hatua ya mwanzo ya vidonda au michubuko tumboni.Maelezo yako si ya kutosha.D alili mojawapo ni maumivu ya tumbo eneo la chembe kama kunawaka moto,ukila chakula tumbo linavuruga na gesi kwa wingi.kubeua na kujamba.Maumivu yanaendana na vyakula vya aina fulani.km chai,kahawa,ndimu,pilipili na vyakula vyenye viungo.Watu wa namna hii inawezekana wakawa na tabia ya kutokuwa na muda maalum wa kula.Ili kupata nafuu...acha vyakula vyenye asili ya ukali,kula mda maalum,tumia na antiacid km magnesiamu au dawa km Relcer Gel km hakuha hata maziwa husaidia.Unahitaji kwenda kwa Daktari upimwe kujua chanzo ni nn.Bakteria aina ya H.pylori husababisha pia.Ugua oole