SoC02 Nikimaliza ngazi hii ya elimu

SoC02 Nikimaliza ngazi hii ya elimu

Stories of Change - 2022 Competition

Ibrah james

New Member
Joined
Jul 20, 2021
Posts
4
Reaction score
3
Vijana wengi hujiuliza ni nini nifanye baada ya kumaliza elimu yangu , haijalishi elimu ya ngazi gani japokua walengwa hasa ni wanao maliza kidato cha nne na vyuo katika ngazi mbali mbali, Lengo kubwa ni kutengeneza maisha bora kwa vijana wanao maliza ngazi za elimu husika, hii ni kwa kujishughulisha katika mambo mbali mbali kama vipaji , elimu walio somea na mambo ambayo yapo katika mzunguko wa jamii kwa muda huo , ni nini vijana wanatakiwa kujifunza na kufanya katika muda wao wa kumaliza elimu ili kutumia muda wao wakiwa nyumbani:

Matumizi ya kipaji ulicho nacho , jamii ya sasa kila kitu kina thaman hivyo inawezesha kijana kutumia kipaji chake katika kutengeneza jina na pesa ili kukidhi mahitaji , mfano mzuri kijana mmoja alikua na kipaji cha kuchora akiwa shuleni kupitia kuchora picha mbali mbali za elimu shuleni ilimfanya ajifunze zaidi na kuanza kuchora picha za sanaa hii ilipelekea kijana huyu baada ya kumaliza kidato cha nne kupata tenda kubwa za kuchora na kujilikana sehemu mbali mbali ila kielimu aliendelea kusomea udaktari lakini kipaji chake bado anacho kutokana na anavyokutumia hivyo sio rahisi kupotea

Kubali kujifunza kwenye fursa mbali mbali ,vijana wanaweza kujifunza fursa mbali mbali wakiwa katika mashule Yao ili baada ya elimu kuweza kujiendeleza au kutekeleza mafunzo waliyo pewa , fursa zipo mbali mbali kama kilimo, biashara na ,zingine ila cha kuzingatia ni kwamba fursa ipi itakua rahisi kwako katika swala zima la kutekeleza , kilimo kama inavyojulikana inakua na mwanzo mgumu ila matunda yake pia inategemea na juhudi zako, kwenye swala la biashara siku hizi kila kitu kinafanyika mtandaon hii inamrahisishia kijana kufanya biashara zake mtandaoni "online " ,pia masoko ya mtandao maarufu kama "crypto currency" pia ni fursa nzuri kwa vijana kujifunza na kujipatia kipato.

Usiache kujaribu , katika maisha yako ondoa neno "siwezi" hili neno hufunga kila linalowezekana hivyo basi kwa kila fursa au jambo linalokuja mbele yako usiache kujaribu , endapo utaona halina manufaa basi hauna budi kuachana nalo ,ukiweza kufanya hivi basi itakua rahisi kugundua ni nn unaweza kufanya na nn huwezi kufanya, mfano mzuri ni kijana mwenye kipaji au kupenda kufanya graphics design na upigaji picha , alipo maliza kusoma kidato cha nne alijaribu kufanya kazi mbali mbali na kuonesha jamii nini anaweza. Hatimae jamii ndogo inayo mzunguka imepokea vizur wazo lake na kumpa ushirikiano , na mpaka leo kija hajakata tamaa na kuingia katika fursa mbali mbali kujaribu bila kusita

Tengeneza vikundi chanya ukiwa nyumbani, muda ambao upo nyumbani jaribu kuunganisha marafiki wenye faida ili kuweza kutengeneza wazo moja zuri ambalo lita leta faida kwa wote , epuka matumizi mabaya ya muda hii namaanisha kutumia muda mwingi katika shughuli zisizo za lazima, hii itakujenga umakini katika kutayarisha kitu bora zaidi na kuweza kuwakilisha katika jamii hata kuleta maendeleo pia , marafiki katika kikundi chenu wanaweza wakawa mchango mkubwa sana katika kufanikisha wazo lako lengwa

Wekeza mapema, kwa kuweka lengo lako katika maendeleo lazima uwe na mtaji au pesa ya kuendesha baadhi ya mambo katika wazo lako hii inatakiwa kuanza kuekeza mapema ili kuweka mtazamo Mzuri baadae, hii inawezekanaje? Kwa mtu mwenye uwezekano mdogo wa kupata pesa basi epuka matumizi makubwa ya pesa na maisha ya gharama ili kuweza kuekeza na kwenye uwezekano mkubwa wa kupata pesa basi wekeza kadili uwezavyo ili kuwa na mfuko binafsi wa kujikimu na kufanya maendeleo yako binafsi na kuendeleza jamii pia.

Vijana wanaopambana katika kutengeneza maisha yao pia kuleta maendeleo katika jamii ,kutokana na maisha yao huwa na mchango mkubwa katika jamii , mfano wa kijana millard Ayo ni maarufu nchini Tanzania katika kutoa habari zenye uhakika na ukweli hii ni kutokana na juhudi alizozifanya toka hapo alipomaliza elimu yake na kuanzisha chaneli yake binafsi na kutokea kufanya vizuri nchini .

Hivyo basi , vijana wanatakiwa kufunguka akili na kuweza kufanya vitu chanya vyenye uchochezi katika kuleta maendeleo kwenye jamii, hii itaongeza kipato pia kuondoa tatizo la ajira kwani kila mtu ana jambo lake analoweza kufanya ila hana mwanzo mzuri au ushauri mzuri wa kuanza kutekeleza jambo lake .

IMG_20220706_230442_789.jpg
 
Upvote 0
Back
Top Bottom