Mimi Diana na watanzania wengi tunataka kumpa kura Dr. Slaa oct.2010 lakini najiuliza nikimpa atatawala vipi huku wabunge wengi watatoka CCM? sitaki kuichezea kura yangu na watu wengi wanajiuliza swali hili naomba watu wa Chadema watueleze tukimchagua atavunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine au atapitisha vipi miswada yake bungeni.Hii mbio ya kuingia ikulu cannot be an end by itself.
Diana
Asante kwa hoja yako.
Slaa akishinda atahakikisha kwamba, kwanza, anapunguza gharama za matumizi ya serikali kwa kuunda mfumo wa utawala wenye wizara chache, ili kuwa na mawaziri wachache, hata kama ni wa CCM. Hii itasababisha kupungua kwa bajeti ya serikali, ambayo imesheheni matumizi yasiyo ya lazima, kama vile ununuzi wa magari ya mawaziri - Toyota LandCruiser VX - ambayo yana gharama kubwa sana, licha ya kwamba kila mwaka wa uchaguzi wananunua magari mapya, ambayo pia yanahitaji mafuta, matengenezo, n.k.
Pia, Slaa nadhani amesema kwamba atahakikisha kwamba kutakua hakuna kitu kinaitwa Mkuu wa Mkoa. Yapo mengi ameyasema, lakini cha msingi ni kwamba, ataweka wazi milango yake, kwamba hata wewe - mwananchi wa kawaida - utakuwa na nafasi yako ya kusema jinsi nchi yako itakavyoendeshwa, kwani, kwa sasa, CCM haijafungua mlango huo wa wananchi kuwasiliana na rais wao moja kwa moja, kumshauri jinsi ya kuendesha nchi.
Slaa anataka Serikali Shirikishi. Kikwete hataki Serikali Shirikishi. Hii ni moja ya tofauti za msingi za kukufanya wewe uendelee na msimamo wako wa kumpa Slaa kura yako mwaka huu!
Asante kwa kumuunga mkono Dk. Slaa!
Tulete mabadiliko YA KWELI!
-> Mwana wa Haki