Nikinywa maji ya babu simpi tena mume wangu

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
MUME MWANGU SI MWAMINIFU KABISA NA DAWA YA BABU AMESEMA UKIWA NA NGOMA UKINYWA IKATOKA UKIRUDIA NGONO OVER..HAYA NDOA VS BABU AMBILIKILE

Wakati Mchungaji akizungumzia hilo, mwanamke mmoja ambaye alikuwa akimsikiliza alikimbia na kwenda kuwaeleza wanawake wenzake ambao walikuwa kwenye gari kwamba "babu amasema kama ukirudia ngono na kisha ukapata tena UKIMWI huponi, mimi nikirudi simpi mume wangu kwa sababu alikuwa siyo muaminifu bora niachike," alisema.

Bw. Said Athumani yeye alisema kwamba haoni sababu ya watu kuendeleza tena tendo la ngono hovyo wakati amepona na kushauri watu watulie katika ndoa zao kwa sababu dawa hiyo imekuja

HUYU NAE NDOA ZENYEWE AZITAKI KUTULIA WATULIE WAPI JAMANI??
 
Si ampeleke huyo mumewe naye akapate kikombe...!!
 
Ndugu ndoa isikie kwa mwenzio wengine hata msikitini/kanisani shida iwe LOLIONDO
we acha tu labda akinywa ayasemeehe maji yampeleke Mumewe
 
simply ni kwamba baada ya kutoka kwa babu mwendo ni talaka tu. au vinginevyo muende wote mkapige cups za mchungaji.
 
binafsi kuondoa haya maneno nimeona niende na familia mwisho wa mwezi haya masharti ayachelewi kuvunja ndoa za watu..unamtuma mkeo kwa aman na upendo akirudi hny mie mmmh labda ukanywe maji kwa yale maisha uliokuwa nayo yapi ukuyaona sikuzote amabakilile akuonyeshe leo??
 
Na iwe hivyo tu kwani ukipona toka kwenye domo la mamba sidhani kama unaweza kurudia kucheza kwenye maji yenye mamba.
 
kama kweli dawa ya babu inatibu ukimwi,hiyo chance haiji mara 2,hata ingekuwa mimi,kama nimeponyeshwa,na mwanamme kicheche,ndoa ningeisamehe.maisha matamu jamani.na ningekuwa single maisha
 
Msihofu hilo ni suala la muda'dawa ya kutibu ukimwi moja kwa moja haipo,babu anasaidia kupunguza kwa muda tu!
 
mimi nadhani hutapona kama ukifanya ngono, na kufanya ngono ni kutoka nje ya ndoa. Inawezekana ukiambukizwa na mwenzi wako ndani ya ndoa ukarudia dawa na ukapona!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…