kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,832
- 4,070
Salaam
Nimekaa nimefungua Diary yangu nimepitia pitia mara nikakutana na budget niliyoiandaa kwa mshahara wangu wa kwanza baada ya kuanza kazi. Nikagundua kumbe nilikuwa na utaratibu wa kuandika matumizi ya Kila mwezi na kiasi ninachokiacha kama akiba lakini nilikuja kuachana na utaratibu huo.
Sikuwa mtu wa kuandika Sana matukio kwenye diary ingawa yaliwepo machache kama kumbukumbu binafsi za maisha yangu.
Naakachana nalo nikashika diary nyingine ambayo hii ni baada ya kuwa na uzoefu katika kazi.
Ndani yake kulikuwa na kumbukumbu za matukio mbalimbali, kumbukumbu za vikao mbalimbali nilivyoshiriki lakini pia niliandika kuhusu malengo yangu ya muda mrefu na muda mfupi.
Mpaka sasa nimekuta nimetekeleza baadhi ya malengo mengine bado yako pending. Kwenye kipengele hiki Cha mikakati binafsi juu ya maisha yangu ndo kipengele mahsusi ambacho nimekaa nikajiuliza kama ikitokea nikaokota diary ya mtu huenda ikawa na manufaa zaidi kuliko yaliyomo kwenye diary yangu ama?
Je,wewe unaandika nini kwenye diary yako?
Ukipoteza diary yako,itakuathiri kiasi gani katika mishe mishe zako?