Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimenunua epson printer L800 na hapa mjini studio zinasafisha picha kwa tsh 200 picha ya size 4 kwa 6, je mimi nikisafisha kwa 200 nitapata faida? Msaada wadau
- Faida utapata tena kubwa tu
- Sababu cost za uendeshaji ni ndogo sana
- Ninapo zungumzia cost za uendeshaji hapa nazungumzia ghalama ya ununuzi wa wino na ghalama ya ununuzi wa karatasi
- Tazama hii picha kwanza
![]()
Karatasi za Picha
Wino
- Utapata kwa tsh 3'000 au 4'000 kwa dar es salaam
- Huwa zinakuwa karatasi 20
- Karatasi moja utatoa picha nne (4) za 4 x 6
- Hivyo idadi ya picha ni 4 x 20 = Picha 80
- Upande wa Fedha utakayopata 80 x tsh 200 = tsh 16'000 [ Hapo faida ni tsh 12'000 ]
Itafikia mahala - baada ya biashara kuchanganya mahesabu itakuwa ni karatasi tu, sababu sifa kubwa ya hii printer epson L800 ni kutotumia wino sana, hivyo hutofikiria unuaji wa wino.
- Ni tsh 6'000 kwa chupa ndogo ya ml 70
- Na ni tsh 10'000 - 16'000 kwa chupa ya ml 250
- Kwa kazi ya printing picha kwa kila siku wastani wa picha 240 wino utajaza mara moja kwa kila miezi mitatu hadi minne (4)
Kwa kifupi - umenunua printer sahihi kwa kazi ya kusafisha picha za aina zote - HONGERA
Ahsante sana mkuu, pia naomba unisaidie eti baada ya huu wino ambao nilinunulia na printer ambao chupa zake zimeandikwa kabisa epson kuishe, je ni aina gani tena ya wino wa kurefill inafaa? Na je ni aina gani ya paper inafaa kwa ubora? Msaada mkuu
Mkuu Mwl.RCT
Swali kwako, hizo karatisi nadhani ni za A4, unawezje kuprint picha 4 za 4*6 ? mimi naprint picha 2 tu za 4*6 kwenye karatsi ya A4, Mkuu kama una utaalam na hili naomba unipe elimu,
Ahsante
Asante mkuu Mwl.RCT nimekupata,
ila mimi ninazo karatasi za 4*6 ambazo zinakuja zimekatwa tayari, naona ni rahisi kufanya hivyo.
simply asking hii printer inuuzwa shilling ngapi????????????????
- Ndio, inaweza kutoa
Mkuu naomba hili swali tulielekeze kwa Mwl.RCT nadhani ana ujuzi mzuri kuhusu hii printer.Mkuu naomba unipe elimu kidogo kuhusu wino mchafu kwenye printer ya epson l 800, namaana kwamba ninapotumia kuna sehemu ya wino mchafu unahifadhiwa? Tuanzie hapo kwanza