Nikishakula ugali huwa sifanyi haya

Black ma colour

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
733
Reaction score
663
Habari

Mimi ndugu yenu nikishakula ugali wa dona na
dagaa vumbi , hakika huwa sifanyi yafuatayo nikiingia JF.

1. Huwa si comment hovyo hovyo

2. Huwa simjibu mtu kwa dharau kisa tunatumia fake ID

3. Mara nyingi huwa nakuwa msomaji na huwa najifunza mengi.

4. Huwa naheshimu mawazo, michango, na biashara za watu.

5. Sipendi kujikuza na kutaka kuonekana na mimi ni boss ihali naishi chini ya dollar 5 kwa siku so Hyatt legency hotel sio viwanja vyangu.

6. Naheshimu watu wenye imani na mitazamo tofauti na mimi.

7. Mimi kutumia tecno na kupata jero la bundle hainifanyi kucomment hovyo hovyo haswa kwa thread ambazo zinahitaji critical thinking .

8. Nakili wazi ile JF ya 2005-2010 hivi imeniathiri sana kisaikolojia, yani kichwa changu bado kinaamini watumiaji ni wale wale ila nikisoma comment na thread nahisi nina usingizi bado.


Nawatakia maombolezo mema ya mtanzania mwenzetu R. A. Mengi

Ts me black ma colour
 

Hongera mkuu kwa kushiba tuombee na sisi tushibe labda tutafanya uyafanyayo

Ila ile jf natamani irudi pia majukwaa yaliyokua yanatembelewa kwa wingi ni intelligence matangazo kilimo na ufugaji jf doctor garage
Ila cku hizi mmu jokes na chitchat ndo yamejaa
 
Watumiaji wamebadilika, wenye umri fulani ndio wengi, wenye akili fulani hawapendi kubishana na wenye akili daraja lileeee
 
Kwahiyo tunaokula dagaa hatupaswi kuwa na "makeke" humu?
 
Kwa hiyo siku ukila wali samaki na kusukumizia na mtindi, hapa hapatatosha siyo? Bora uendelee kula hivohivo
 
Kwa hiyo siku ukila wali samaki na kusukumizia na mtindi, hapa hapatatosha siyo? Bora uendelee kula hivohivo
Mkuu siku nikila mlo huo hakika dunia nzima itanitambua vyema. Sitojali mkubwa wala mdogo, niyawajibu kwa upana na marefu mtajuta kunitambua
 
Heshima ni kitu cha muhimu sana. Ule au usile kitu, ule kwa gharama au kwa kawaida , uvae vizuri au vibaya ila heshimu kila mtu.

Amini usiamini wanao-comment hapa ndiyo hawa hawa unaopishana nao njiani na mjini na kwenye daladala.

Kama unavyowaheshimu huko basi hata hapa jukwaani waheshimu pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…