Ni kweli unaweza kuwa kama shy-rose. lakini tahadhali nzuri nyingine ni kwamba unaweza utafute kazi uchelewe kuipata, au uipate ukute mazingira yake yanakupa kichefuchefu. Siku hizi tunashauri vijana kuwaza pia uwezekano wa kubuni biashara binafsi. Ukisoma PR na Marketing biashara yako binafsi itapaa kama tai.
Katika kozi yako watakufundisha jinsi ya kumtambua mteja wako, watakufundisha jinsi ya kutambua matamanio na mahitaji halisi ya mteja wa biashara yako, jinsi ya kuposition biashara yako, na jinsi ya kupamba biashara yako kwa maneno na matendo. Big-up man. umechagua kozi nzuri sana. Na kazi lazima utapata tu; ya kwako binafsi, au ya kuajiriwa.