Nikita Kering Aishinda Tuzo Ya AFRIMMA 2026

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312

Mwimbaji wa Kenya Nikita Kering’ ameshinda tuzo ya Best Female East Africa katika African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2026 iliyofanyika Dallas, Texas, Marekani.
Ushindi huo unamfanya kuwa Mkenya pekee kushinda tuzo katika hafla ya mwaka huu.

Kering’ aliwashinda wasanii wenzake wa Kenya NjeRae na Bridgit Blue, pamoja na Zuchu na Abigail Chams kutoka Tanzania.
Tuzo hiyo pia imefikisha idadi ya tuzo zake za AFRIMMA hadi tano, baada ya kushinda mara mbili mwaka 2019 na mara mbili tena mwaka 2021.

Ushindi huo unajiri muda mfupi baada ya kutoa EP yake mpya, The Lick Back. Hakuhudhuria hafla hiyo Dallas, lakini aliwashukuru mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii.
 

Attachments

  • 5ae41c88-b5f0-4eb4-81bb-70df09b87c3b.webp
    29.3 KB · Views: 15
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…