Nikitumia Jogoo la kuroiler kupandisha kwa tetea wa kienyeji mayai yatatamiwa na kutotolewa?

Joined
Mar 9, 2016
Posts
41
Reaction score
17
Habari za kazi waungwana.

Samahani naomba kufahamu jambo hili linanitatiza kidogo.

Hivi endapo nitatumia majogoo ya kuku chotara aina ya kuroilers kupandisha mitetea wangu wa kienyeji, majike ya kizazi kitachopatikana yatakuwa na uwezo wa kuatamia hadi kuangua mayai?

Shukrani za awali.
 
Lengo lako ni kupata kuku anaetamia mayai?

Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni kuenzi utaduni tu. Huwez kuweka malengo nao. Wanataga wakijisikia.

Mwingine anaweza tamia mayai 15 akatoa 10/6/9 vyovyote. Ukuaji wao ni fixed.

Wafuge kwa malengo ya kuwa nao nyumbani lakini usiweke malengo ya kibiashara
 
Lengo langu hapa ni kupata kienyeji walio improved sasa nahofia huenda nikapoteza sifa yao ya kuatamia.
 
Lengo langu hapa ni kupata kienyeji walio improved sasa nahofia huenda nikapoteza sifa yao ya kuatamia.
Keanu
 
Kiongozi hii me hua naifanya sana wanatoka kuku ambao kwa 75% ni kienyeji na wanastamia vizuri tu
Shukrani Sana kaka. Nimesoma andiko moja kwamba majike huwa yanapoteza sifa ya kuatamia na kwamba hata akiatamia ana kuwa hana consistency nzuri anaweza ishia njiani kwa mfano. Vipi haijawahi tokea kwako hii?
 
Yah wanalalia
 
Mie wa kwangu wanalala, japo wengine wanataga kwa muda mrefu zaidi. Anafiksha mpaka mayai 19!
 
Shukrani Sana kaka. Nimesoma andiko moja kwamba majike huwa yanapoteza sifa ya kuatamia na kwamba hata akiatamia ana kuwa hana consistency nzuri anaweza ishia njiani kwa mfano. Vipi haijawahi tokea kwako hii?
Niliwahi kufanya hivyo nikagundua kwamba kuna kuku jike amekua akitaga kwazaidi ya wiki tatu na hajawahi kuatamia
 
vipi collabo ya jike kienyeji dume saso na dume liwe la kienyeji jike liwe la chotara saso au kroila ukitotolesha kizazi kinachofuata kinakuaje
 
vipi collabo ya jike kienyeji dume saso na dume liwe la kienyeji jike liwe la chotara saso au kroila ukitotolesha kizazi kinachofuata kinakuaje
Niliwahi kupandisha tetea la kienyeji na chotara,
nikapata matetea mawili na jogoo moja, vingine vilichukuliwa na paka wakabaki hao watatu.
Tetea moja kwa mara ya kwanza lilitaga mayai 21 akaatamia vizuri na kuangua vifaranga 11.
Kimbembe mara ya pili alitaga nonstop karibu miezi mi4 hakuna kuatamia tena,
 
duuuu
 
Aisee😂😂
 
Kama huna mashine ya kutotolea vifaranga (hatchery) weka mayai kwenye kapu lenye pumba yapate joto. Hesabu siku zikifika 25-28 angalia mayai kila siku yanaweza kutoa vifaranga na wafe kwa kukosa hewa.
 
Ahsante bibi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…