Nikiulizwa Magufuli ameacha nini kikubwa, nitasema kuwa Magufuli ameacha hofu kwa Watanzania

Mwenyezi Mungu aliona watu wake wanateswa na mtu mmoja akaonelea ni kheri ampeleke motoni mapema ili waja wake wasiendelee kuteseka.
Huo ndio ukweli acheni mbwembwe za kijinga
Hivi unaamini huu upuuzi? Wewe ukifa Mwenyezi Mungu atakuwa na sababu gani ya kuchukua?
 
Naunga mkono hoja...nnachoshukuru Ni kuwa mungu ametusikia kilio chetu..
 
Umetumia maneno makali na ya jumla kumuita kila aliyemkubali JPM kuwa ni mjinga. Pesa alizokuwa anatembea nazo hayati ni sehemu ya pesa za matumizi ambazo ni sehemu ya bajeti ya rais ya mengineyo (miscellaneous).

Wengine huzitumia kununua mikufu ya dhahabu, wengine huzitumia kuhongea warembo wa mijini na wengine ndio kama JPM kuwasaidia maskini na ujenzi wa shule na vyoo kila alipokuwa akipita.

JPM alikuwa ni mzalendo kwa maana ya kujitoa kufanya miradi mikubwa kwa kubana matumizi na kupambana mpaka anahakikisha inamalizika. Kama sio kuweka msisitizo maalum ile terminal ya uwanja wa Ndege isingemalizika.

Kama sio kuweka msisitizo kikazi, ndege zilizoifufua ATCL zisingenunuliwa hata moja, barabara na madaraja mengi yasingejengwa.

Kila binadamu anao upande mbaya na upande mwema. JPM alizikwa na kinamama wengi mpaka wakatandaza kanga njiani ni ishara ya upande wake mwema.
 
Ameacha hofu kwa mafisadi, wavivu, wala rushwa, vyeti feki, wadhulumaji, wakwepa kodi, wapiga madili, magaidi
Ongeza na hli ameacha hofu kwa viongoz ambao wanatumia ghalama kubwa kubadili nyeupe kuwa nyeusi, na chakula kitamu alichoacha watu wamejisahidia nyuma ya nyumba ili ile harufu mbaya ya kinyesi ikichafue, ila haiwezekani,
 
Kweli hofu kwa mafisadi,wenye vyeti feki, Msoga gang.

Ila kwa wananchi aliondoa hofu, eti mtu anakuja na vitisho eti wimbi sijui langapi.Watu wanadunda tu.
Eti chanjo,watu hawachanjwi na maisha yanasonga.
Hofu ipo awamu hii ya mipasho ukimzingua nae anakuzingua lazma uwe mpole hata kama haki ni yako.
 
Magufuli kaacha smetuaribia taifa kiujumla. Kaacha amelemaza taasisi zote za nchi. Hiyo hofu aliyoacha mfano wake ni Ile iliyoachwa na biashara ya utumwa katika bara la Afrika ambayo ulikuwa inatishia uwepo wa Waafrika ktk ulimwenguni.
Nimeshakugongea LIKE mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…