Nikki wa Pili ataja vipaumbele vyake 8 siku akiwa Rais

Makuhani

Senior Member
Joined
Oct 9, 2017
Posts
103
Reaction score
39
Msanii wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameeleza vipaumbele vyake nane iwapo siku moja atakuwa Rais wa nchi.


1. Kikaoo kikubwa cha serikali yangu sio baraza la mawaziri itakuwa mkutano mkuu wa kijiji/ mtaaa (kitaa kinaongea)

2. Kipimo cha maendeleo kitakuwa kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi, makusanyo au shilingi.

3. Mfumo wa elimu utajikita kupima “learning” yani kujifunza sio kupima ufaulu na ufeli

4. Vyama vyenye nguvu vitakavyo kuwa vinafanya mikutano na kuihoji serikali sio vyama vya siasa bali vyama vya wakulima, wafanyakazi, walimu, machinga, boda boda, madaktari nakadhalika.

5. Serikali itakuwa mdau namba moja kwenye uchumi na mwekezaji atakuwa mkulima, mfugaji, mchimbaji mdogo, wavuvi wadogo na wafanyabiashara wa wadogo.

6. Ardhi, elimu, maji, afya havitakuwa bidhaa bali hifadhi ya jamii.

7. Maisha bila maadili hayana mana kila mtoto lazima afundishwe kuwa na adabu, uaminifu, heshima, ujamii, upendo, bidiii na kujiamini.

8. Mahusiano na mataifa ya Afrika, hakutakuwa na neno wahamiaji haramu, Mwafrika hawezi kuwa haramu Afrika ni nyumbani kwao.

Hata hivyo ameleeza kuwa maswali ataulizwa wakati wa kampeni ukifika lakini akiwa kama mgombea binafsi.

Source: Bongo5
 
Iko safi ila tatizo la huyu akiwa raisi atakuwa much know
 
Vyama vyenye nguvu vitakavyo kuwa vinafanya mikutano na kuihoji serikali sio vyama vya siasa bali vyama vya wakulima, wafanyakazi, walimu, machinga, boda boda, madaktari nakadhalika.
Kwahiyo vyama vya siasa havitakua na kazi
 
Mdogo wangu Nikki, hujawahi kuwa hata monitor wa darasani toka umeanza chekechekea mpaka unamaliza chuo kikuu. Hiyo ni ishara kuwa huna karama ya uongozi, kazana kuimba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…