Nikki Wapili: Swala la Wasanii kulipwa Na TV/Radio Stations

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Habari Wakuu

Ni Kama siku moja imepita tangu Msanii Nikki Wapili apost picha ya yeye akiwa na Wazari wa Habari utamaduni na Michezo,Mzee wa Goli La mkono Mh.Nape Nauye katika ukurasa wake wa Instagram

Akisema imeshakamilika kuwa kuanzia Januari Moja wasanii watakuwa wanalipwa na vituo vya Radio na Runinga hapa nchini kwa vile vituo vitakavyo kuwa vinacheza nyimbo za wasanii wabongo!

Means zimebaki siku Kama 13 hivi hio sheria ianze kufanya kazi na kwa utawala huu Wa Magufuli najua wataisimamia Sana

Nacho jiuliza ni kwamba hili litawezekana vipi kwa vigezo vifuatavyo

1) Je wamiliki wa hivyo vituo wataweza? Ilihali kulipa kodi tuu wanasumbua mpaka wakimbizane na TCRA?

Pia hata kuwalipa mishahara ya wafanyakazi wao ni tatizo

2) Hii inamaana Gani kwa muziki wetu wa Bongo unao kua Ilihali wasanii wana tegemea Sana media Hasa TV stations na Radio stations kukuza mziki wao?

3) Vipi kuhusu undergrounds je nao itatakiwa walipwe au itakua ni kwa msanii anayependa kulipwa tuu?

Na Kama ni kwa wasanii wote Je inamaanisha itakuwa basi sasa kwa undergrounds kusikika na kuonekana katika Vituo hivyo au hapo imekaaje?

4) Naona Kama mziki wa mbele utakuwa unapewa Sana Promo kwasasa kuliko hata mziki wetu na tutawasikia na kuwaona Hadi maunderground wa Marekani hadi China sababu Mmiliki gani atakae penda kupata hasara?

Madhara ya hii ni kuwa utamaduni wetu hauta kua Bali tutakuza utamaduni wa Nchi za watu

5) Je Niki na muheshimiwa pale Kati wanamanisha na kwa nyimbo za Dini au Ni kwa Bongofleva Tuuu

Mwisho sijui Kama wamewashirikisha wadau wa mziki katika hili ila kwa upande wangu Naona Kama WAMEKURUPUKA Kwa lugha nyepesi hili ni mapema Sana kwa nchi Kama yetu ambayo uchumi wake ni wa chini sanaa

Kwanini wasisimamie mengine kwanza kabla ya hili Kama vile kuburn CD,Matangazo Yale ya tunaweka nyimbo kwenye Flash!

Pia ni mda wa wasanii wetu wabongo kujituma na kufanya Mziki mzuri Ili show ziwe zinawalipa kuliko hili walilo kuja Nalo!
 
Post ya Nikki
 

Attachments

  • 1450387556633.jpg
    29.2 KB · Views: 263
Chadema mbona hamba jema kwa hiyo mnatakaje nchi hii?
 
Na sisi wapiga mnanda tutalipwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…