Nikki Wapili: Swala la Wasanii kulipwa Na TV/Radio Stations

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Habari Wakuu

Ni Kama siku moja imepita tangu Msanii Nikki Wapili apost picha ya yeye akiwa na Wazari wa Habari utamaduni na Michezo,Mzee wa Goli La mkono Mh.Nape Nauye katika ukurasa wake wa Instagram

Akisema imeshakamilika kuwa kuanzia Januari Moja wasanii watakuwa wanalipwa na vituo vya Radio na Runinga hapa nchini kwa vile vituo vitakavyo kuwa vinacheza nyimbo za wasanii wabongo!

Means zimebaki siku Kama 13 hivi hio sheria ianze kufanya kazi na kwa utawala huu Wa Magufuli najua wataisimamia Sana

Nacho jiuliza ni kwamba hili litawezekana vipi kwa vigezo vifuatavyo

1) Je wamiliki wa hivyo vituo wataweza? Ilihali kulipa kodi tuu wanasumbua mpaka wakimbizane na TCRA?

Pia hata kuwalipa mishahara ya wafanyakazi wao ni tatizo

2) Hii inamaana Gani kwa muziki wetu wa Bongo unao kua Ilihali wasanii wana tegemea Sana media Hasa TV stations na Radio stations kukuza mziki wao?

3) Vipi kuhusu undergrounds je nao itatakiwa walipwe au itakua ni kwa msanii anayependa kulipwa tuu?

Na Kama ni kwa wasanii wote Je inamaanisha itakuwa basi sasa kwa undergrounds kusikika na kuonekana katika Vituo hivyo au hapo imekaaje?

4) Naona Kama mziki wa mbele utakuwa unapewa Sana Promo kwasasa kuliko hata mziki wetu na tutawasikia na kuwaona Hadi maunderground wa Marekani hadi China sababu Mmiliki gani atakae penda kupata hasara?

Madhara ya hii ni kuwa utamaduni wetu hauta kua Bali tutakuza utamaduni wa Nchi za watu

5) Je Niki na muheshimiwa pale Kati wanamanisha na kwa nyimbo za Dini au Ni kwa Bongofleva Tuuu

Mwisho sijui Kama wamewashirikisha wadau wa mziki katika hili ila kwa upande wangu Naona Kama WAMEKURUPUKA Kwa lugha nyepesi hili ni mapema Sana kwa nchi Kama yetu ambayo uchumi wake ni wa chini sanaa

Kwanini wasisimamie mengine kwanza kabla ya hili Kama vile kuburn CD,Matangazo Yale ya tunaweka nyimbo kwenye Flash!

Pia ni mda wa wasanii wetu wabongo kujituma na kufanya Mziki mzuri Ili show ziwe zinawalipa kuliko hili walilo kuja Nalo!
 
Hili Suala wapo sahihi kabisaa, na Binafsi naliunga Mkono 100%

Kitakachofanyika ni kuwa Redio na Tv zitapewa muongozo wa kusema 70% au 60% ya content ziwe ni za kibongo, kisha redio nazo zitakachofanya ni kuongeza bei za matangazo yao, ndo ksema kwamba kama voda alikuwa anatangaza dk 5 kwa lki 5 basi itaongezeka kidogo. So suala la redio kumudu kulipa na mziki kushuka linakuwa limesoviwa hivyo.

Ishu ya kwamba Redio zinashindwa kulipa watangazaji ,si kweli, yamkini ni wao binafsi tu kutaka Super normal profits, na kama biashara ingekuwa haiwalipi si wabadilishe??

Undergrounds na wasanii wengine, watalazimika kuwork hard, sababu kazi sasa zitapigwa kwa ubora wa kazi, na si kwa sababu nyingine, na kama wananchi watarequest (demand ikiwa kubwa) hakuna mtu atakae zuia wimbo wako kupigwa,

Na kwa sababu saiv kuna njia nyingi za kupromote kazi ya msanii, inamaana msanii akitoa kazi atakuwa na jukumu la kuhakikisha inazifikia vituo vya redio na TV kisha kufanya promo kupitia njia nyingine mf Social nertworks au hata kupitia Redio n TV halafu kisha jamii ikubali wimbo na awe na airtime ya kutosha.

Hili suala pia litarahishsia serikali kufuatilia mapato yaote yanayotokana na Entertainment Industry na kuyalipisha kodi stahik
 
Hapo kwa undergrounds bado tunadanganyana, it will be hard for them to be heard hata Kama nyimbo ina ubora. Tumeshuhudia wasanii wengi wakibaniwa promo mpaka watoe pesa hata Kama ngoma ni kali.
We should have a new plan for undergrounds
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…