Niko dillema, naomba mawazo yako

Ww ni mwanaume kuendelea kulelewa na mwanaume utakuja ujikute umeloa nyuma oooh namuamin anaweza kupitiwa yule ni binadamu nenda kijijin kafanye kazi
Hana hiyo dirty mind, ila wewe pekee yako
 
Kwa nini mshangazi? Kwa hiyo unataka amwache ili tuongeze singo maza mtaani? Wacha hizo mkuu! Aende kwa mzazi mwenzake waendeleze gurudumu bwana!
 
Inaonekana wewe ni wale watu wanaopenda kulelewa.
Kuendelea kujitolea ni kupoteza muda halafu kukaa kwa mshikaji muda mrefu sio vizuri.
Mzazi mwenzako amekupa ramani nzuri kabisa sehemu ambayo utaenda kupambana kwa jasho na Damu upate chochote sio kwamba huko amekuita akakuhudumie kama ulivyozoea. kafanye kazi ndungu usichezee hiyo bahati Kuliko kukaa Dar kupoteza muda na kuongezea watu mzigo. Kafanye kazi.
 
Rudi njombe kalime
 
b
bro nenda njombe kwa mkeo then komaa na kilimo you never know MUNGU amekuandalia nini kaka amini kwamba
 
Moyo unasema niende akili inaniambia baki, moyo unasema baki akili inaniambia Nenda🙌
mkuu kachaa chini na mshkaji wako ongea nae kirafiki mpe mpango wako wa kupambana kwa kilimo ukiwa karibu na wife wako kwa masalahi mapana ya familia na yako binafsi jamaa ako ni muelewa atakuelewa na mahusiano yenu hayataharibika easy
 
Dar ni kama center ya michongo.

Haramu na halali yote ipo hapo.

Just make sure you listen, connect with the right people na uache kuongea sana.

Ukiwa unatoka nje ya Dar uwe na ramani kama siyo hivyo Dar ni best option.

Hata ukiamua kua mshona viatu, mshona viatu wa Dar hafanani na mshona viatu wa Kinyanambo C.
 
Umemshauri vizuri, afikirie juu ya huu ushauri 📌📌📌
 
Kwa nini mshangazi? Kwa hiyo unataka amwache ili tuongeze singo maza mtaani? Wacha hizo mkuu! Aende kwa mzazi mwenzake waendeleze gurudumu bwana!
Mwanaume unamshauri mwanaume mwenzio "aende" kwa mwanamke hiyo yenyewe ina-sound kupoteza miliki na utawala, siku zote mwanamke ndio anatakiwa "kwenda" kwa mumewe

Singo maza sio kichaka cha kupoteza power ya kuwa mwanaume otherwise aende akalelewe tu
 
Sasa wewe mkuu unamshauri aendelee kufugwa hapo kwa jamaa?
 
Sasa wewe mkuu unamshauri aendelee kufugwa hapo kwa jamaa?
Kwa jamaa hafugwi wala kulelewa hapo anapambana wanaume huwaga hatuna masimango kama wanawake.

Kuna kipindi jamaa angu aliona kwao wanamtumia tu anauza duka la kaka ake bila future yoyote, akaja magetoni tukawa tunachill wote tunapika na kula kipindi hicho mm napiga kitabu chuo, alikuwa akijishughulisha na mbaga za uwakala hadi akapata pa kushikia na akapanga geto lake mwanzoni nilikuwa nikimbust na boom langu lakin akajichanga akawa na kwake

Huyo jamaa aache mbaga za kuajiriwa na kujitolea, mtaani pesa ipo kuanza ni kugumu ila ukishazoea mwaka unaweza usifike unamiliki geto na mazaga mengine mjini hapa. Hapo sasa hata akimuita mzazi mwenzie atakuwa kifua mbele kuliko akaenda kutegemea mshahara wa uyo manzi ataletewa michepuko hadi usiku wa manane na asiweze kusema chochote
 
Nafurahi pale mtu anapotaka ushauri wa alime yaan afanye kilimo ama kazi.
Be a man bro rudi huko jishushe na umwambie mambo ya shamba akuachie na wewe upambane kweli. Coz nnavyojua hautakuwa ati wewe ndio wa kwenda kulima wewe ni kusimamia tu watu wakifanya kazi. Usiamini ke hawezi kukusaidia ndugu yangu she can na utaboa bora tu asiwe mshangazi. My friend kwanza huko kijijin ndo pazuri coz hujulikani. Utakuja kujulikana after kuwa umelima hata misimu (sio minokia na misamsung)miwili. Na mungu akakusaidia ukapata mazao na bei ikawa nzuri i swear hutakumbuka kuajiriwa ndugu yangu. Mwambie huyo unayeishi kwake akupe nauli kama hauna na uende huko bro na utanishukuru baadae.
 
Mkuu mbn adabu yako ni ndogo - jitahidi kuwa na busara si kila mahali ni pakutukana, haikupandishi ila inakushusha. Fanya hivyo itakusaidia 🙏
Wewe unachepuka na unataka kuheshimiwa tena.
Hata hujui uende wapi ukiitwa maraya si heshima hiyo
 
Mimi nakwambia kama ana nguvu kule atateseka mwaka mmoja tu uchumi utarudi na atammiliki huyo mwanamke na ki mshahara chake cha ualimu! Kule Njombe kuna maneno mwaka mzima wanapiga kazi za shamba! Hivyo kwa mwaka anaweza kuvuna mara 2 au 3!
 
Mimi nakwambia kama ana nguvu kule atateseka mwaka mmoja tu uchumi utarudi na atammiliki huyo mwanamke na ki mshahara chake cha ualimu! Kule Njombe kuna maneno mwaka mzima wanapiga kazi za shamba! Hivyo kwa mwaka anaweza kuvuna mara 2 au 3!
Aje atupe mrejesho hapo baadae
 
Huu ndo ukweli watu wengi hawajui kuhusu Dar, ukishindwa Dar seemu nyingine kutoboa si rahisi labda ufanye kilimo😇
 
Mimi nakwambia kama ana nguvu kule atateseka mwaka mmoja tu uchumi utarudi na atammiliki huyo mwanamke na ki mshahara chake cha ualimu! Kule Njombe kuna maneno mwaka mzima wanapiga kazi za shamba! Hivyo kwa mwaka anaweza kuvuna mara 2 au 3!
Nimepanga kujitoa sadaka 1/2 years kwenye kilimo na biashara
Biashara ya kununua bidhaa kwa jumla mjini nasambaza vijijini au mtaani kwenye maduka madogo madogo/ stationery ntafanya online application kama
TIN no.
Death & Birth certificate
Bima
Inshort Nina ujuzi wa kutumia kompyuta vizuri na mimi nina pc-mchawi hapa ni router
Nimplan hizi zitakuwa side hustle zangu kilimo ndo priority
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…