Niko na mzigo wa nguo lakini frem sina. Nifanyeje

ladyvvvv

Member
Joined
Feb 7, 2017
Posts
6
Reaction score
8
Naomba Ushauri jinsi ambavyo nitaweza kuuza nguo zote bila kuwa na frem. Niko dar
 
Jaribu kuuzia hapohapo unapoishi, au pitisha vyuoni kwenye hostel za kike. Instagram account nayo unaweza kuitumia kuuzia
 
pitisha vyuoni..tafuta mtu unayemjua kwemye maoffice akuungishe na wafanyakazi anaowafanya naon..weka facebook na ista..Pitisha door to doors na kwenye saloon..
 
Mkuu kamwage kariakoo, yani ukiona sehemu yeyote yenye mkusanyiko we mwaga mzigo Mkuu

Mzee wa Fent Ford si aliruhusu kufanya biashara sehemu yeyote
 
Huo mzigo umenunua mwenyewe au umepewa!? Maana haaiingii akilini ununue bidhaa usijue utauzia wapi!!

Anyway, mimi nakushauri kama ungeweza utembeze mitaani, kama mzigo ni wa vijana (kinadada na kinakaka) ungepeleka hata vyuoni!!

Ukishindwa kabisa basi uuze kwa wauzaji wadogo wadogo... Yaani upige mnada mahali!!

Nawakilisha.
 
Hapo hapo kwako... Ziweke kwenye hanger vizuri nyuma ukiwa umeweka kitambaa kizuri...

Zipige picha... Alafu anaza kuzipost kwenye social media zote ulizopo...mwanzo mgumu ila watakuzoea na utaanza kuuza...

Naona watu wakifanya hayo...

Cc: mahondaw
 
Tatizo inaonekana mitandao ya kijamii hi huitumii vizuri kujiingizia kipato mana najua Instagram, facebook unazo sasa kama unazitumia hizo vizuri basi duka utaona halina umuhimu lakini kama unatumia kwa kubadilisha profile picture pole..pia jaribu door to door business ambayo unawatembelea majirani na hata mitaa ya jirani kwa kuwaonyesha bidhaa zako ila hutakiwi kuwa na aibu.
Angalizo; usijaribu kukubali uwakopeshe watu wa mtaani utalia bora uuze uwe unachukua faida ndogo
 
Niliagiza kwa ajili ya kuuza ila mambo yameingiliana nimeshindwa kulipia frem bei sana kariakoo milioni kwenda juu
Mzigo umetoka china moja kwa moja
 
Piga picha sambaza. Nenda ktk hosteli zote za vyuo ktk mkoa uliopo omba ruhusa kwa mlinzi getini ingia ndani gonga milango fanya biashara watoto wapate msosi usikae na mzigo mkuu.
 
Pole Ndugu, ila jua Jf ni wateja pia

Wateja wangu wakubwa ni JF na members wa ma group ya Whatsapp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…