Niko na swali

Okoth p'Bitek

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2019
Posts
1,124
Reaction score
1,384
Kama malaika Gabriel alimtokea Mariam na kumwambia utapata mtoto Kwa uwezo wa roho mtakatifu na jina lake utamuita yesu na atakuja Kwa ajili ya kuikombia Dunia....


Tusome hapa kidogo

Wazazi wake walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii.

Swali langu ni kwamba inakuwaje biological mother wa mkombozi wa Dunia anasahau majukumu aliyoachiwa na malaika wa Mungu kuhusu mwanae atakayeikomboa Dunia...

Imo Jesus was just a scholar
 
Hizo ni hadithi mkuu ni za kutunga
 
Mkuu amesahau vipi majukumu yake? Unamaana kumchunga mtoto au
 
Mkuu amesahau vipi majukumu yake? Unamaana kumchunga mtoto au
Japo kwenye amri za Musa Kuna mahala wanasema usijijengee sanamu ya kuchonga...

But can you imagine Mama wa kitanzania au wa kiyahudi anatokewa na Malaika Kisha anaambiwa utapata mtoto Kwa uwezo wa roho mtakatifu na utamwita yesu...na huyu mtoto ataikomboa Dunia

Kesho mzazi yule yule anamkuta mtoto anatimiza kile mama yake alichoambiwa na Malaika kwamba ndio jukumu la mwanae, halafu bado anamuuliza mwanae unafanya nini hapa tumekuwa tukikutafuta Mimi na baba yako and Jesus ghafla anaonekana mwenye hasira na kuwajibu wazazi wake Kwa ghadhabu..refer the strory.....why is this happening? Je ni kwamba Jesus na Mama yake Kwa ujumla were not aware of the mission proceeded by God..
 
Afu hizo siku 3 zote katoweka alikuwa anakula wapi msosi? Kwani alikuwa na maokoto? Alilala wapi na hakuwa na ghetto?

Afu kwanini Mungu hakumuua tu shetani ili kumaliza bifu kuliko mlolongo mrefu mpaka akamtoa mwanae adedishwe kwa ajili yetu? Simple tu, kill satan case closed
 
Mungu anataka na nyie muende motoni milele
 
Lakini according to historians ni kweli yesu alikuwepo.
Wanahistoria wamebaki na swali kubwa sana kuhusu habari ya kufufuka kwake.ikionekana ni habari ambayo ina discrepancy nyingi sana.

Kufufuka kwake ni suala la kiimani ila kihistoria lina mikanganyiko mingi.
 
Biashara za watu hizo mzee
 
Swali langu ni kwamba inakuwaje biological mother wa mkombozi wa Dunia anasahau majukumu aliyoachiwa na malaika wa Mungu kuhusu mwanae atakayeikomboa Dunia...
Inaonekana mariamu alikuwa mtu wa vaibu hivyo ikapelekea kutojali mambo ya msingi
 
Una maanisha mungu alisahaulika sasa kwanini mungu hasijuwe kama wenzake wanaondoka
 
Kumbuka Yesu ni "Mungu kweli" na ni "mtu kamili". Kuna wakati alifanya matendo ya kibinadamu kam aulivyo mimi na wewe, na wazazi wake walimulewa hivyo
!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…