Ndoa maana yake nini? kama maana yake financia comfort and unconditional love from one side basi mkubalie huyo wa kwanza. Kama maana yake struggling (financialy and emotionaly) together and finding comfort in mutual love basi mchague huyo wa pili.
in the end utakuwa na John while una cheat na Peter lol
Hakuna anaye kufaa hapo.
Ana kasoro nyingine ambazo umeamua kutoziweka adharani nadhani ni kasoro kubwa ndio maana umeona hata nourma kuzianika hapa
Mkuu mwenzangu,
Niko hai hai, naitwa na wajukuu niwasaidie wasitoane macho. Nimeweza kusoma posts 2 tu, ile ya mleta mada na hii ya kwako.
Sina objection...John is my big choice....Maisha hayahitaji pressure kama hizo za Peter.
Ila mbaya zaidi na kadri ya kwa principles zangu, si jambo zuri mdada kuolewa na mdogo wake.
Nitarudi tena asubuhi kuwasalimia......
Babu DC!!
Haya haya haya........... Kongosho where are you @? Kura ya tatu na ya mwisho ya Veto ishamuangukuia Pita. We utakuwa matron kwa harusi ya Da Asia. Mi ntaukwaa ubestman wakati babu mwenzangu DC atakuwa mshenga. Ikumbukwe kuwa sauti ya DC ni sauti ya mungu mdogo.
Leo saa 11 jioni tukutane Fyatanga kwa ajili ya kikao cha maandalizi. Ukizingatia kuwa Da Asia ni bikira, harusi lazima ifanyikie Ikulu ndogo.
narudi badae kidogo
Nilisema ntarudi sababu nilikuwa nakumbuka hii story hapo chini, nadhani huyu ni Peter.
Si kila mwanamme anaweza ndoa, Peter ulishampa nafasi na akashindwa kuitumia, je unadhani sasa kaenda okota wapi akili ya kuwa mume?
Endelea na John, mapenzi yatajiset huko huko mkiwa ndani, wakati mwingine tunajifunza kupenda.
Really Kongosho tunajifunza kupenda hata kama hatupendi? Si vema kufanya mkataba na mtu usiyempenda na si vema kufanya mkataba na mtu asiyeeleweka. Hapo aingie barabarani tu na kuendelea kutega antena zake vizuri
Ndahani, bora akatege antena barabarani upya.
Ila kumbuka, husband materials ni wachache mno ila kama anaweza kula hata akina 'marioo' aanze kuasaka.
Angekuwa hampendi kabisa asingemtatiza.
Ningekushauri umkubali Peter lakini maelezo yako ya sababu za nyie kuachana na wakati wote mliumia hayaingii akilini
Je kama wote ni watu wa hasira mnadhani mtadumu kwenye ndoa?
Huyo mwenye kids wala sikushauri, ingawa inawezekana hata Peter ana watoto si alikuwa na mke au yeye hakuzaa. Na umesema Peter ni mdogo kwako; uoni hiyo ni sababu ya yeye kukudengulia na kwenda kuoa wa umri wake yalipomshinda ndio anakukumbuka. Be careful. Asijekuwa anakurudia umlee.
Jaribu kutafuta kwingine; achana nao wote.
"Kuna mwingine, huyu namuita Peter. Peter yeye, tuliwahi kua na mahusiano miaka kama mitano iliyopita ambayo yalidumu kama miaka miwili na kiasi fulani. Tulipendana sana mpaka tulipewa majina mji huu. tukatofautiana kidogo sana na kitu cha kijinga mno, sababu ya kila mmoja kua na hasira na mwenzie, tuka break-up. niliumia na yeye naamini aliumia sana"
samstevie, pesa ya John wala hainiweki njia panda, maana hapa nilipo kwa sasa niko juu kiasi fulani and not because of him. kama nilivyosema mwanzo, nina maisha yangu mazuri tu kwa effort yangu mwenyewe. namshukuru mungu sijawahi kuishi kwa kufanyiwa bali najifanyia mwenyewe, upo sam...?
umenena vyema kama peter ana watoto na maisha yake ni ya kuungaunga pia kwako ni mdogo kiumri hapo anatafuta mteremko loh! Hakufai jaribu kumfikiria upya John kama ataweza kukaa rohoni pia naona bahati yako ni mbaya jaribu upya kutafuta mwenza achana nao wote.Nyumba kubwa kukufafanulia tu ni kuwa wote wana watoto. John anaishi na watoto wake. Peter nae ana watoto lakini wanaishi na mama yao. kwa sasa yeye anaishi mwenyewe ila anasomesha watoto wake wakiwa kwa mama yao, pamoja na matumizi anatoa.