Niko njia panda nahitaji msaada wa haraka sana

Kama amejuta msamehe,ila ujue fimbo ya mbali........Hili linaweza kurudia tena na tena kutokana na umbali.
 
Mpige chini huyo jamaa afu uje kwangu, yaani watoto wazuri wenye mapenzi ya ukweli kama nyie wanazingua? Sie wengine kila siku tunaangukia pua kwenye choices, kudadadeki..!
Piga chini huyo...!😛ainkiller:
 
Mpige chini huyo jamaa afu uje kwangu, yaani watoto wazuri wenye mapenzi ya ukweli kama nyie wanazingua? Sie wengine kila siku tunaangukia pua kwenye choices, kudadadeki..!
Piga chini huyo...!😛ainkiller:

Asnte kwa mawazo yako kaka, tulia na mwombe Mungu atakusaidia kumpata yule mtakayependana na kuheshimiana kwa dhati
 
 
Aiseee! Wanaume si watu.
Muulize sababu iliyomfanya amtongoze rachel wakati yupo na wewe. Sababu ya kuacha na rachel na sababu zinazomfanya arudi kwako. Kama sababu zake zinaridhisha msamehe na mrudiane. Bora huyo kawa muwazi, unaweza ukaangukia kwa njemba lingine likawa hovyooo.
 
mmmh mimi naona usimkubali maana hajatulia wala hana mapenzi ya dhatikwanza unajua ameachana na rachel kwa sababu gani?je kama ni rachel kamuacha kwa sababu ya msichana mwingine tena?una uhakika upo na rachel tu hapo?usikubali kuwa spare tyre tafakari chukua hatua
 
Kabla ya kumsamehe make kitako muongee na kufikiria kwa nini hicho kimetokea. Muongelee pia future plans. Kama distance ndio ilimuangusha, na kama mna mipango ya baadae mmoja wenu atafute kazi kwenye mkoa wa mwenzie. Sijasema uache kazi, utafute kazi kwanza ndo uhame. Then unaweza kumsamehe, masharti na vigezo kuzingatiwa.
 
Wewe si unamjua vizuri mtu wako?
Je asingekueleza ukweli ulkua tayari kuachana nae???
Angeweza hata asikuambie na ukumbuke kwamba
Mimi nakushauri umsamehe ila kwa makubaliano maalum maana anatakiwa awe na msimamo! anatikwa ajue kama anakupenda au bado ana mpango wa kuendelea kuchaguachaguaaaaaaaaaa
Asije kukupotezea muda na kukuacha pabaya zaidi!
 
Huyo kaka anaonesha km mkweli vile, maana mpaka akuambie uchafu wake wote ambao angeweza kunyamaza na usiujue, labda amejisikia kuumia kw kutenda dhambi kwaiyo anatubu kwako, ila all in all kujua reason ya kuachana kwao ni muhimu sana!
 
Mimi nina mtazamo tofauti, Huyo jamaa atakuwa ni mzinzi na siyo muaminifu kabisa anatakiwa apate mzinzi mwenzake.Inawezekana ikawa aliangukia mikononi mwa msichana kicheche akatendwa then akaamua kurudi kwako.Cha msingi muombe Mungu akusaidie upate mume bora.Ukimuachia Mungu kila kitu mume au mke bora anakuja mwenyewe Automatically.
 

husinyo hata kama nitamuuliza na akanieleza itanisaidia nini si nitaendelea kuumia tu?
 
Eeeh? Yaani alikuchukia ghafla na akachana picha zako na kuchoma moto zawadi zote ulizomtumia???? Kweli mapenzi kizunguzungu! Mi nimechoka ghafla na ngoja nisishauri chochote kwa sasa. Mweeeh!
 
Pole sana lola kwa hayo, ila mimi nina mawazo tofauti kidogo!

Huyo bf wako anasema ameachana na Rachel kwa muda huu, Je nini kilichomfanya aachane nae na aje kwako kukiri na kuomba msamaha. Yawezekana pia Rachel anampenda sana bf wako, huoni nae anaweza kwenda kuomba msamaha kwa bf ili warudiane kama zamani??
Hawa wanaume ni vigeugeu ipo siku atamkumbuka halafu atamuomba kuonja "kuduuu nae" kwani wewe upo mbali na anajua wewe ni vigumu kufahamu hilo. Kaa chini fikiria na hili pia!
 
husinyo hata kama nitamuuliza na akanieleza itanisaidia nini si nitaendelea kuumia tu?

Muda mwingine ni bora kuujua ukweli ili kama una mapungufu yoyote ujirekebishe kama vile bf anavyotaka, kwani hakuna binadamu mkamilifu kila mtu ana mapungufu yake.
 
Aiseee! Wanaume si watu.

Kama sababu zake zinaridhisha msamehe na mrudiane.

Bora huyo kawa muwazi,

lingine likawa hovyooo.

wanaume ni watu bila sisi msingekuwepo!

Sababu lazima ziwe na uzito hata machozi jamaa atamwaga ili mradi arudi

akuna cha uwazi hapo hiyo zuga amka lola, romance walifanyia wapi maneno mbofumbofu na ili winter la chuga aaghrrr

mhhh kuna wanawake wanahasira na wanaume maneno makal sana
 
dah,labda alikujaribu,sitaki kuamamini jamaa ni mjinga kiasi hicho!muendelee tu,toa simu katika flight mode na iweke kwenye daladala mode
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…