Dada yako alijua anatembea na mume wa mtu?
Dada yako ana kipato cha kikidhi masha yake? ili kujua kama ni u-gold digger umemponza
Ushauri usijaribu kumkataza baba mtoto asije muona mwanae au asishiriki katika makuzi ya mtoto unaweza kuja juta pindi utakapoulizwa baba yangu yupo wapi na mtoto i mean atakayekuwa anadhulumiwa haki yake hapa ni mtoto kukosa upendo wa baba na kukosa makuzi ya baba.
Haina kuchukia hapa ita wote na kujadili jinsi ya kushirikiana kumlea mtoto
na huyo dada yako mbona hujamchukia? wote wametenda dhambi usimuadhibu mtoto kwa kukosa malezi yababa. Kosa lmetendeka mwachie mwanaume alete matunzo ila mwambiie dada yako aache uhusiano wa kimapenzi
Ningefurahi kama angenielewa akavunja hiyo affair,ila anadai inabidi waendelee kuwa pamoja for the sake of their baby.
Kwa hiyo wewe you don't care for the sake of their baby?
(mwenyewe unajua jinsi mlivyo waongo),
hivi nyinyi mnazungumza kutoka dunia ipi?????
tanzania yetu kuna mila na dini ambazo mwanaume anaruhusiwa kuwa na
mwanamke zaidi ya moja.......
sasa kama ni maamuzi yao.wewe yanakuuma vipi?????
hivi mwanao akija kuzaa na mume wa mtu utafanyaje??????
unafiki unakusumbua....
hivi nini maana ya ku cheat kama mtu dini au mila za kwao
zinamruhusu kuwa na wake zaidi ya mmoja???????
wewe unataka dunia hii watu waishi kama unavyoamini wewe?
wewe utaweza kuishi kama watu wengine wanavyo amini?????????
Nimekuelewa Dena nami sitaki kuwaingilia kwa walichoamua. Kinachonikwaza ni kuwa sitaki kumtambua kama shemeji na kushirikiana nae kuhudumia mzazi maana dada anataka aje kwangu baada ya kujifungua mpaka atakapo recover.
Nimeshamweleza kuwa sijapenda alichofanya ila anahitaji sana msaada wangu atakapojifungua.
Sioni sababu ya kumchukia huyo mwanaume kwani huyo dada yako alijua ni mume wa mtu na akaamua kuzaa nae. Chakumsaidia umlazimishe huyo mwanaume awe na wake wawili kwani alijua ana mke na akawa na dada yako, asijitetee chochote. kama aliweza kuwa na mkewe na dada yako kwa wakati mmoja aendelee tu mimba isiwe sababu ya kumuacha kwani alivyokuwa anafanya bila kinga alitegemea nini? Mlazimishe aoe.
Bi dada, mdogo wako ndio kashaamua hivyo huna jinsi lazima mshirikiane kumuhudumia mzazi unavyochukia hivyo ina maana unamkosea mtoto ambae hana hatia haki ya kuhudumiwa na baba yake.
Ila honestly mdogo wako ndio mwenye makosa kama mtu wa kumchukia hapo ni mdogo wako, alikua anajua fika huyu ni mume wa mtu na inavyoonyesha yeye mwenyewe ndio ameamua kujibebesha hiyo mimba makusudi (samahani kama nitakuudhi), kwani mwenye uamuzi wa kuzaa ni mdogo wako na si huyo mume so kama umeamua kumsaidia mdogo wako alieamua kubeba mimba ya mume wa mtu kwa hiyari sioni sababu ya kumchukia huyo mbaba wa watu.
Tena ushukuru kama amekubali kuhudumia hiyo mimba na mtoto, kwani angekua mwingine ndio ingekua umemfukuza hivyo.