Niko njiapanda ya kuchagua dini sahihi


Chakuku shauri kwanza zingatia maandiko 📖 ya dini husika mimi naanza na neno “Uislamu” linatokana na neno la Kiarabu “Islam” lenye maana ya "kujitoa/kujisalimisha kwa Allah kwa utiifu kamili" kwa kumpwekesha katika kila jambo na Uislamu unamaanisha “kunyenyekea kwa mapenzi mbele ya Mwenyezi Mungu” kwa "Tawhidi" kumpwekesha yeye Allah kwa kumtii na kuacha maasi.

Katika Qur'an
Surah Aali ‘Imran 3:19
"Hakika Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu...".
Na katika Hadithi:
Hadithi ya Jibril (Imepokewa na Muslim)
Mtume (s.a.w) alisema:
"Uislamu ni kushuhudia kuwa hakuna Mungu ila Allah na Muhammad ni Mtume Wake kuswali swala tano kutoa Zaka kufunga Ramadhani na kwenda Hija kwa mwenye uwezo".

Mwanazuoni Shaykhul-Islam Ibn Taymiyyah alisema:
"Uislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu kwa "Tawhidi" na kunyenyekea Kwake kwa utiifu na kujitenga na Shirki na wenye kushirikisha".
Na katika Surah Aali ‘Imran 3:85
Allah anasema "Na atakayefuata dini isiyokuwa Uislamu basi haitakubaliwa kwake..."
 
Yesu alikuwa Muislam
UONGO konki huu,
Hadi Yesu anaondoka duniani uislamu ulikuwa haujaasisiwa na Wakatoliki kupitia mtu wao Mudi.

Na Yesu angekuwa Kobaz asingeongelea habari za kuanzisha Kanisa lake..

Mathayo 16:
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

 
Hakuna dini sahihi Ila dini ni UPENDO na kujipenda na kupenda watu.

Ukifanya hivyo utamuona Mungu .
 
Umeongea vizuri sana mkuu lakini ni jambo la ajabu kwamaoni yangu eti kuinyamazisha akili yako eti iwe na ukomo wa kufikiri
 
Sasa tuambie Yesu alikuwa dini gani
Mimi nasubiri hapa utuambie 📢 na Ukristo ni Project ya nani
 
Dini zote ni sawa,kila moja ni bora kulingana na muamini wake.
Hata huo Ukristo upo wa aina Pana aliouacha Yesu Kristo na Pana ulioanzishwa na mazayuni movement toka nchi za Magharibi kwa lengo la kuwabrainwash wakristo vipofu wa sasa waitukuze Israel ili kufanikisha ajenda ya kupush New Israel kama taifa.
IS-RA-EL
IS .... ISIS Mungu jua
RA.... Mungu mwezi
El... Mungu Elshadai.
Maana ya Israel ni Muunganiko wa Jua,mwezi na Mungu ndo tafsiri ya alama ya nyota kwenye bendera yao
 
Umeongea vizuri sana mkuu lakini ni jambo la ajabu kwamaoni yangu eti kuinyamazisha akili yako eti iwe na ukomo wa kufikiri
Utofauti wa binadamu na viumbe wengine ndio hiyo.....UDADISI
Ukimuondolea udadisi binadamu atakuwa sawa na wanyama wengine tu

Binadamu ataendelea tu kudadisi...... Wataalamu wanatuambia kuhusu hii dunia tu binadamu anaijua chini ya asilimia 20 tu kuhusu Dunia tunayoishi
Na kuhusu Ulimwengu asilimia anazojua ni chini 0.01

Kama nilivyoandika kuna dhana mbili, Imani imemtengeneza Mungu na Sayansi imetengeneza Theories

Soma maandiko ya dini kuhusu uumbaji utagundua muandishi alikua hajui lolote kuhusu dunia na ulimwengu kama tuujuavyo leo

Lakini ukisoma theories za kisayansi angala zinasapoti ulimwengu tuujuavyo leo ingawa nazi bado zinaacha maswali yasio jibika

So usikubali kuwa mtumwa wa imani fulani kwasababu haujui ninani kaumba ulimwengu
Tunajikuta tumezaliwa tu kisha tutadadisi na tutakufa na kucha udadisi ukiendele
Ukizaliwa China na wazazi wachina unakua Budha, Ukiwa India unaasilimia kubwa kuwa Muhindu, Ukizaliwa viunga vya Teheran Unakua Mshia, Ukizaliwa na Muhadzabe unakua unaabudu mapango, ukizaliwa Roma utakua mkatoliko, ukizaliwa Tel Aviv utakua Myahudi na ukizaliwa Dunia ya tatu kama Tz itategemea wakoloni wa dini gani walipiga kambi mkoa uliozaliwa na mababu zako wakakolonishwa dini hiyo na wewe ukakuirithi
 
Nakubali mkuu
 
Ooooh! Kumbe Yesu dini yake ilikuwa ukristo?

Vipi kuhusu Ibrahim, Isaka na Yakobo walikuwa na dini gani?
 
Shida unapotaka kulazimisha watu wafuate imani fulani kisa tu wao ni asili fulani, imani haipo hivyo. Imani sio sawa kabila kwamba kwa sababu baba yako ni msukuma basi na wewe kabila lako ni msukuma.

Hao waarabu walikuwa na imani za mababu zao pia kabla ya kuletewa uislamu na ndio maana kuna muda hadi panga zilitumika maana kuna waliyokuwa wakizuia huo uislamu kusambaa maana wenyewe walikuwa wanafuata imani za mababu zao.
 
Kwanini mnaona ni sahihi kufuata imani tu ambazo waliamini wazee wetu bila kufikiri kwamba hizo zilikuwa ni imani ambazo zilikuwepo katika wakati wao tu? Hata hao waarabu kama wasingeletewa uislamu pengine hadi sasa wangekuwa wanaabudu masanamu ndio zilikuwa imani za mababu zao pia.
 
Hakuna MUNGU.

Hakuna DINI sahihi.

Dini ZOTE ni UTAPELI.


Emancipate yourself from mental slavery.

Trash God.

Trash Religion.

Live free.
Hakuna live free hata wewe kuna mambo na mitazamo unalazimika kuishikilia kwa sababu ni atheist.
 
Achana na ujinga huo..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…