Niko sahihi au?


kwahiyo unataku nini?? uambiwe uko sahihi au usaidiwe au usifiwe??

Pole sana,
 
salma jaribu kuwa mkweli kwa moyo wako! baada ya kupitia yote hapo juu ni KAMA VILE WEWE MWENYEWE UNAIJUA SABABU YA MAMBO haya yote!
- unasema unamuona kichefuchefu ilihali mnaishi nyumba moja!!!
-anaijali familia shida tu ni kwamba hana muda wa kukaa na familia yake....-INAWEZEKANA KUNA KERO UNAMPA SASA ANASHINDWA KUWA NA WEWE WAKAT WOTE
-ANGALIA ISIJE KUWA ULIHARIBU MWENYEWE SASA UNATAKA KUM BWAGIA ZIGO MUMEO!!!
-WANAUME HAWAPENDI MANENO WALA HAWAPENDI MASHINDANO TUMIA BUSARA NA SI HASIRA NA KIBURI ILI UIRUDISHE NYUMBA YAKO KATIKA AMANI
 
Mi naona Salma kwakuwa mlifunga ndoa kanisani ni vyema ukawashirikisha viongozi wa kiroho katika hili suala lako aisee kwasababu kulingana na maelezo yako inaonekana wazi wewe na mumeo wote hampendi ndugu zenu wajue shida inayondelea katika familia yenu.Nakwakuwa we mwenyewe umekiri kwamba bado mko pamoja sababu ya mtoto chukua hatua ya kuwashirikisha viongozi wa dini haraka kabla huyo kijana wenu hajaanza kuwauliza maswali yasiyojibika.
 
hapana sijamaanisha ulichosema ila nimejaribu kukufanulia kuwa si mzee kiasi cha mimi kumuona kichefuchefu ila ni matendo yake ya kuudhi na kukera

Ana kukera nini tuweke wazi tukusaidie sisi tulivyo kuelewa ndo hivyo kutokana na maelezo yako.
Mbona matumizi anakupa umekubali na vile vile akiwa na kiu anajua jinsi ya kukupata sasa kero ipi tena?
 
Ana kukera nini tuweke wazi tukusaidie sisi tulivyo kuelewa ndo hivyo kutokana na maelezo yako.
Mbona matumizi anakupa umekubali na vile vile akiwa na kiu anajua jinsi ya kukupata sasa kero ipi tena?
mhh mpendwa hakuna mahali nimesema kuwa akiwa na kiu anajua mahali pa kunipata...nazungumzia tatizo la yeye kutojua nini maana ya familia
 
nashukuru mpendwa,tutafanya hivyo
 

1.Nahisi hiyo red ya mwisho ndo inafanya mme wako anakuwa jinsi alivo,una kiburi sana
2.inasikitisha kwamba umefunga ndoa kanisani,limetokea tatizo kama hili hujui kwamba unapaswa kwend kumuona mchungaji,padri etc kusolve tatizo lenu
3.namba 2 hapo juu,utawezaje kwenda kumuona mchungaji wakati mwenyewe una kiburi? nadhani hata kanisani huendi una jihubiria mwenyewe chumbani

Pole sana,lakini naona una lazimisha kuingia ndani kila siku kwa kupitia dirishani na kuna mlango.
kama ulivosema,uko na mmeo sababu ya mtoto tu,nahisi yeye mwenyewe anatamani saivi ndo angekua ana chumbia
 
unanihukumu mpendwa kwa kusema nna kiburi...kuhusu mchungaji kiukweli mpaka sasa nilikuwa najidanganya kuwa atabadilika leo,kesho masiku yanakata ila nnalazimika kulifasnyia kazi hilo kwa sasa,umeniacha kidogo hapo mwisho kwenye msamiati
 
Pole sana. Usijali mwanao kuitwa mtoto wa mama. Play your part. Maisha yatamsaidia kumjenga upande wa pili. Inaonekana baada ya magomvi na kusuluhishana, mumeo bado ana lake rohoni hajalisamehe.

Anyway, ni maisha yenu lakini sababu ya kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya mtoto, si jambo jema. Hasa, kesi yenu yajionyesha wazi hampendani, hamuheshimiani na kubwa kuliko yote mlishindwa kusameheana hapo awali. Mnavyozidi kukaa pamoja, mnaongezeana chuki tu.

Kila la heri.
 
unanihukumu mpendwa kwa kusema nna kiburi...kuhusu mchungaji kiukweli mpaka sasa nilikuwa najidanganya kuwa atabadilika leo,kesho masiku yanakata ila nnalazimika kulifasnyia kazi hilo kwa sasa,umeniacha kidogo hapo mwisho kwenye msamiati

4years unajiandaa kwenda kwa mpatanishi wa kiroho?
 
unanihukumu mpendwa kwa kusema nna kiburi...kuhusu mchungaji kiukweli mpaka sasa nilikuwa najidanganya kuwa atabadilika leo,kesho masiku yanakata ila nnalazimika kulifasnyia kazi hilo kwa sasa,umeniacha kidogo hapo mwisho kwenye msamiati

...dont take it personal. Hakuna awezaye kukuhukumu humu jf, ukweli unaujua wewe na mw'mungu wako. Chukulia michango na maoni ya wachangiaji kama changamoto watu wamekuelewa vipi. Sote tuna mapungufu yetu humu.
 
4years unajiandaa kwenda kwa mpatanishi wa kiroho?

Hapo kuna jambo, dada anataka kuvunja ndoa, kafanya vituko aachwe hajaachwa. Sasa anatafuta sababu ya kuacha.

Huyu mama/dada anataka kubomoa na hapa anatafuta symphathy. Tatizo hapa ni yeye mwenyewe, asuke au anyoe at herr own risk.

JF tunatoa ushauri wa kujenga na si kubomoa; na ushauri huo unatolewa kuendana na tatizo lenyewe, tunasema ukweli unaostahiki. Ila kwako mleta mada tatizo ni wewe narudia tena, unachofanya si sahihi.
 
Mhhhh! Ndoa hizi jamani!!! Miaka minne!!! Duh! pole sana Salma.
 


SHOSTI
wewe, acha kabisa kuchezea akili za watu, halafu vile Mungu si Athumani umejiumbua mwenyewe. Pamoja na kufuta post, foot print hizo.


$£&&*%$"*&%$
 

Nashangaa hapewi ukweli,..
tena mme wake ni mvumilivu sana na kama unavosema inaonekana kamnyima alichotaka (talaka) mda mrefu sana
 
pole sana dada yangu..upo sawa kabisa na kama ni kichefuchefu ni sawa kabisa potelea mbali, hili tatizo ni mwanaume ndio kanzaisha lazima tukubali. lakini shetani pia amechukua mkondo wake hapo



Hapo kwenye Red Umejuwaje kama tatizo ni la mwanaume? Naona kama mtoa mada hajasema chcoche kilichomfanya mumewe asiwe karibu na familia.

Ameulizwa swali na mchangiaji hapo juu naona analikwepa, Ameulizwa ''Ulishamsaliti mumeo kwa kutoka nje'' hajajibu. Haiwezekani mwanaume aijali familia ya mkewe ila asimjali mkewe lazima mwanamke umechangia kwa njia moja au nyingine kumkimbiza mbali mumewe. Yawezekana na wewe dada unarefusha mabega kutaka uwe kichwa cha nyumba kitu ambacho mumeo hakikubali bali kukupuuza. Labda unaongea sana, mbele ya mtoto wenu unaongea vibaya kumkandya mumeo... hiyo nayo inaweza kufanya mumeo akupuuze maana anaona hujampa nafasi kama baba wa nyumba kila kitu unajifanya ni wewe.

Unasema mumeo anatowa matumizi yote ya familia ila ukaribu tu kwa familia ndo haupo... Haingii akilini kwa mtu wa kuhudumia familia asijali familia dada lazima na wewe kuna kitu ulikifanya kikamuumiza mumeo na hukuomba msamaha au ulifanya jeuri.

Unalalamika wachangiaji wengine wanatoa ushauri wa kukupinga, nadhani ni haki wa wachangiaji kupima maneno uliyotowa na wakatowa comments zao kwa kadili wanavyoelewa. Si lazima wote wakubaliane na wewe hata kama wanaona wewe ndo mwenye matatizo.

Kwa mwanaume kutokuwa karibu na mtoto wako tu kweli ndo kilicho kutowa chumbani na kuamia chumba kingine au kuna lingine hutaki kusema? Kwa mwanamke mcha Mungu usingezigi kuweka gap kiasi hicho na mumeo kwa kukimbia chumba. Kuhama chumba ni kuongeza tatizo zaidi ya kulipunguza. Umehama chumba umepata unafuu wowote hadi leo? Rudi chumbani kwa mumeo, na Ujishushe Uombe samahani kwake umwambie kama kuna kosa ulilifanya basi akusamehe.... hii yote kujionyesha kwake kuwa unampenda na bado unamuhitaji katika maisha yako. Acha jeuri/ukolofi kwa mumeo. Huyo ndo uliyempenda na kukubali awe mumeo,... mapungufu ni ya binadamu, jishushe kwa mumeo na zaidi mpe mumeo nafasi yake kama baba wa familia. Juwa wajibu wako kama mama na umwachie mumeo wajibu wake kwa familia na kwa mtoto.


Zaidi, Muombe Mungu akusamehe kwa mapungu uliyonayo, akailinde ndoa yako na familia yako. Akakuongoze katika kuongea kwako ili usimkwaze mumeo bali ukaongee yale yatakayoijenga ndoa yako.
 
pole sana salma, ila mungu ni mwema ipo siku atabadilika,
kilio chako kiwe ni kwa mola wako, ingawa kuna ukweli unaouweka
kuwa siri.. ila kuna ile sms uliyotuma kuwa akirudi Tanzania kitu
ambacho kimewafanya watu waone kuwa kuna siri kubwa hapo,
kikubwa muombe mungu akupe nguvu za kukabiliana na hali uliyokuwa
nayo,na pia ni vizuri uwajulishe na wazazi wa pande zote mbili hapo
itakusaidia kukupa haueni kidogo,


pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…