Hapo kwenye Red Umejuwaje kama tatizo ni la mwanaume? Naona kama mtoa mada hajasema chcoche kilichomfanya mumewe asiwe karibu na familia.
Ameulizwa swali na mchangiaji hapo juu naona analikwepa, Ameulizwa ''Ulishamsaliti mumeo kwa kutoka nje'' hajajibu. Haiwezekani mwanaume aijali familia ya mkewe ila asimjali mkewe lazima mwanamke umechangia kwa njia moja au nyingine kumkimbiza mbali mumewe. Yawezekana na wewe dada unarefusha mabega kutaka uwe kichwa cha nyumba kitu ambacho mumeo hakikubali bali kukupuuza. Labda unaongea sana, mbele ya mtoto wenu unaongea vibaya kumkandya mumeo... hiyo nayo inaweza kufanya mumeo akupuuze maana anaona hujampa nafasi kama baba wa nyumba kila kitu unajifanya ni wewe.
Unasema mumeo anatowa matumizi yote ya familia ila ukaribu tu kwa familia ndo haupo... Haingii akilini kwa mtu wa kuhudumia familia asijali familia dada lazima na wewe kuna kitu ulikifanya kikamuumiza mumeo na hukuomba msamaha au ulifanya jeuri.
Unalalamika wachangiaji wengine wanatoa ushauri wa kukupinga, nadhani ni haki wa wachangiaji kupima maneno uliyotowa na wakatowa comments zao kwa kadili wanavyoelewa. Si lazima wote wakubaliane na wewe hata kama wanaona wewe ndo mwenye matatizo.
Kwa mwanaume kutokuwa karibu na mtoto wako tu kweli ndo kilicho kutowa chumbani na kuamia chumba kingine au kuna lingine hutaki kusema? Kwa mwanamke mcha Mungu usingezigi kuweka gap kiasi hicho na mumeo kwa kukimbia chumba. Kuhama chumba ni kuongeza tatizo zaidi ya kulipunguza. Umehama chumba umepata unafuu wowote hadi leo? Rudi chumbani kwa mumeo, na Ujishushe Uombe samahani kwake umwambie kama kuna kosa ulilifanya basi akusamehe.... hii yote kujionyesha kwake kuwa unampenda na bado unamuhitaji katika maisha yako. Acha jeuri/ukolofi kwa mumeo. Huyo ndo uliyempenda na kukubali awe mumeo,... mapungufu ni ya binadamu, jishushe kwa mumeo na zaidi mpe mumeo nafasi yake kama baba wa familia. Juwa wajibu wako kama mama na umwachie mumeo wajibu wake kwa familia na kwa mtoto.
Zaidi, Muombe Mungu akusamehe kwa mapungu uliyonayo, akailinde ndoa yako na familia yako. Akakuongoze katika kuongea kwako ili usimkwaze mumeo bali ukaongee yale yatakayoijenga ndoa yako.