'Nikomoeni' ya CCM yaanza kuwatia adabu waliogombea ubunge

'Nikomoeni' ya CCM yaanza kuwatia adabu waliogombea ubunge

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Wooote waliogombea ubunge uwe na sifuri au miaka kadhaa; kwanza hakuna mshahara wa Julai na Agosti bila kujali umerudi kazini tayari, bila kujali ulikuwa masomoni, ulikuwa likizo yako, nk. Najua walimu wako madarasani wakionesha uzalendo wao wa miaka yote kuisaidia CCM. Sasa lazima waandike barua upya ya kuomba likizo isiyo na malipo, baadaye wataandika barua ya kuomba kurudi kazini upya!

Hapo nahisi kuna mtego. Tunajuana nchi hii, bhana! Wanasiasa wameshajimilikisha kazi hiyo kuwa ni yao tu! Wameona sasa wamebomolewa na wasiokuwa ndani ya siasa kwa miaka yote, tatizo limeanza! Au wanawinda nani kaenda kwa ACT, DP, TLP n.k? Yaani kazi zingine zote, nendeni lakini siasa musiguse pamoja na kwamba woote walikuwa watumishi wa serikali hii hii! Nikomoeni hiyo! Endeleeni na uzalendo!
 
Nauliza; Hao mawaziri wanaozunguka wakiwa kazini na wakati ni wagombea wa nafasi hiyo hiyo, na wao wako likizo ya aina hiyo au kuna nini?

Tunahitaji mjadala mkubwa badala ya kutunga sheria mtu akiwa na hisia za kifamilia. Vituko kama hivi Upinzani itakuwa taabu kabisa! Wafanyabiashara nao sijui wanatiwa kibano gani?
 
Nawaonea huruma sana wanasiasa waliokwenda kujaribu kiukweli inauma basi tu
 
Nauliza; Hao mawaziri wanaozunguka wakiwa kazini na wakati ni wagombea wa nafasi hiyo hiyo, na wao wako likizo ya aina hiyo au kuna nini?

Tunahitaji mjadala mkubwa badala ya kutunga sheria mtu akiwa na hisia za kifamilia. Vituko kama hivi Upinzani itakuwa taabu kabisa! Wafanyabiashara nao sijui wanatiwa kibano gani?
Kweli! Nawasikia mawaziri wakitoa hata maagizo na wanakula pesa ya serikali wakiwa wagombea. Utumishi wajitathmini, badala ya kuitikia tu!
 
Kweli! Nawasikia mawaziri wakitoa hata maagizo na wanakula pesa ya serikali wakiwa wagombea. Utumishi wajitathmini, badala ya kuitikia tu!
Sielewi kwa nini mawaziri wako kazini wakati wanagombea.
 
Back
Top Bottom