Habari dada Rebeca,
kwa ushauri wangu mimi kwa kuwa ndo unataka kuanza hiyo aina ya biashara uliyoifikiria, ni vyema ukabadili idea kwa kuwa mtaji wenyewe ni wa kukopa mahali, na kama unavyojua biashara huanza kama mtoto anapozaliwa yaani unahitajika kuwa mvumilivu hadi ikue na kukomaa ( kuanzia miezi 3, miezi 6 hadi mwaka 1). Pili kwa biashara za taxi kwa siku unaweza kupata Tsh 10,000 hadi 20,000 na bajaji ni Tsh 10,000 hadi 15,000 kulingana na hali ya chombo, msimamizi (dereva), mahali zinapofanyia kazi nk.. hivyo kwa hiyo Milioni 6 hata kama ukifanikiwa kupata gari na bajaji nzuri, itakuchukua zaidi ya mwaka hadi miaka miwili kurudisha mtaji.. Una nafasi ya kukopa hadi kiasi gani? kwa riba gani? marejesho ni ya muda gani?..nakushauri fanya biashara hizi zifuatazo kwea huo mtaji (mda mfupi unaweza kurudisha mtaji na kuanza kupata faida):
- Jiko la Bar
- Kibanda kizuri cha kuuza chips
- Choo cha kulipia
- Duka la vyakula
- Duka la jumla
- Kuuza mayai kwa jumla
- Ufugaji wa kuku
- Vipodozi
- Salon ya kiume
- Fast Food Cafe etc etc