NIKOPESHE App ya mikopo, kuna anayeifahamu?

NIKOPESHE App ya mikopo, kuna anayeifahamu?

Misokalya

New Member
Joined
Sep 5, 2020
Posts
2
Reaction score
1
Habari wana JF,

Kuna mtu yeyote humu anayeifahamu au aliyewahi kuitumia hii App ya Nikopeshe?

Wanatoa mikopo bila riba na unachohitaji ni namba ya NIDA tuu.

Ushauri wenu tafadhali.
 
Matapeli hao, Kuna mtu alinieleza eti unalipa 3000 ndo wao wakupe pesa, kibongo bongo hapo utapigwa tu
 
Habari wana JF,

Kuna mtu yeyote humu anayeifahamu au aliyewahi kuitumia hii App ya Nikopeshe?

Wanatoa mikopo bila riba na unachohitaji ni namba ya NIDA tuu.

Ushauri wenu tafadhali.
Too good to be true. Mambo mengine ni kutunia common sense. Hakuna mtu anafanya biashara isiokuwa na faida halafu achukie risk kubwa hivyo.
Unamkopa mtu unayefahamu hadi kwake hakulipi, ije kuwa umkope mtu kisa namba ya Nida na bila riba.
Kawachangie ela ya kuprocess form mkuu
 
Matapeli hao, Kuna mtu alinieleza eti unalipa 3000 ndo wao wakupe pesa, kibongo bongo hapo utapigwa tu
Hao ni matapeli kama walivyo matapeli wengine, kwanza wanakuhadaa usajili majina, namba ya NIDA, ukimaliza kujaza wanakuletea ujumbe kuwa, umekidhi vigezo vya kupata mkopo Tsh 250,000/- bila riba, na kupata hiyo pesa unapaswa uwatumie Tsh,5000 ya fomu, wanakupa namba ya simu utakayo watumia, ukiwatumia tu fasta wanailamba, harafu wanakuletea ujumbe, sasa umekaribia kupata mkopo wako, tuma Tsh,15,000/-ili uidhinishwe rasmi; wamekuwekea Email na namba zao kwa ajili ya mawasiliano kwa msaada zaidi, lkn ukiwatumia email hawajibu, na ukiwapigia simu inasena namba uliyopiga haipo.
 
Back
Top Bottom