Gnyaisa
Member
- Jul 13, 2021
- 23
- 24
Katika BIBLIA kuna maandiko kadhaa yanayoonesha ahadi za Mwenyezi Mungu kwa taifa la Israel pindi alipokuwa akiwatoa utumwani Misri. Ni ahadi ya kuwapeleka katika nchi ya maajabu, nchi inayotiririsha maziwa na asali! Sina uelewa mkubwa katika masuala ya dini na elimu ya jiografia lakini NAKATAA maelezo ya wachambuzi wetu duniani kuhusu ilipo bustani hiyo.
Naamini nchi hiyo ya Mungu haiko Mashariki ya kati bali hapahapa barani Afrika. Naamini Nabii Musa hakupaswa kuvuka bahari ya Shamu na kwenda bara jingine bali alipaswa kuvuka jangwa la Sahara na kuja Mashariki mwa Afrika (Pengine ndio maana safari ilikuwa ya mbinde sana). Bado naamini Tanzania ndilo taifa aliloahidiwa Abrahamu na sisi watanzania (hasa vijana) tuna kila sababu za kujivunia hilo. Hebu tutazame maajabu yafuatayo;
Kwa miaka mingi wanasayansi mbalimbali walikuwa wakizunguka duniani kote kutafuta asili ya binadamu. Wataalamu hawa wa masuala ya jiolojia na historia walizunguka katika mabara yote na mataifa mbalimbali bila mafanikio. Walipiga kambi Mashariki ya Kati lakini hawakuambulia kitu! Baadae wakaamua kuja Afrika ili kukamilisha ushahidi kwamba walitembelea dunia nzima. Mnamo mwaka 1911, mjerumani Wilhelm Kattwinkel alifanikiwa kupiga kambi katika Bonde la Oldupai Gorge nchini Tanzania na kujionea mafuvu mengi ya binadamu wa kale!
Baadae mwaka 1913 mjerumani mwenzake Hans Reck alikuja na timu ya wataalamu ili kujiaminisha lakini vita ya kwanza ya dunia ikasitisha tafiti zao. Miaka kadhaa baadae, magwiji wawili wa sayansi, Louis na Mary Leakey waliithibitishia dunia kwamba binadamu wa kale aliishi katika eneo ambalo kwa sasa ni nchi ya Tanzania zaidi ya miaka milioni moja iliyopita. Mpaka sasa hakuna tafiti mpya za kisayansi zinazopinga hilo.
Mbali na uvumbuzi huo, zipo shahidi mbalimbali za kimazingira zenye kuelezea wazi kwamba taifa letu ni bustani tosha ya Edeni iliyokosa matunzo. Hebu tutazame kwa kifupi;
Sifa kuu ya bustani yoyote ni uwepo wa mandhari yenye kuvutia na viumbe mbalimbali wa asili katika eneo hilo. Tanzania ni taifa pekee duniani lenye viumbe wengi wa asili ambao hawapatikani katika maeneo mengine. Tuna utitiri wa hifadhi za taifa zinazovutia maelfu ya watalii kila mwaka. Tuna hifadhi ya taifa Ruaha (Hifadhi ya pili kwa ukubwa Afrika baada ya Kafue iliyoko Zambia), pia tunayo hifadhi ya taifa Arusha, hifadhi ya taifa Gombe, hifadhi ya taifa Katavi, hifadhi ya taifa Kilimanjaro, hifadhi ya taifa Mahale, hifadhi ya taifa Mikumi, hifadhi ya taifa ziwa Manyara, hifadhi ya taifa Rubondo, hifadhi ya taifa Serengeti, hifadhi ya taifa Saadani, hifadhi ya taifa Tarangire, Hifadhi ya taifa Udzungwa, hifadhi ya taifa Kitulo, hifadhi ya taifa Mkomazi, na hifadhi ya taifa tarajiwa ya Saanane. Hifadhi ya Serengeti pekee ni kubwa kuliko taifa la Gambia!
Katika maajabu saba ya asili ya bara la Afrika, maajabu matatu yanatoka nchini Tanzania huku ajabu la 4 (mto Nile) chimbuko lake likiwa Ziwa Viktoria linalomilikiwa na Tanzania kwa zaidi ya asilimia 50. Hakuna wa kunipinga nikisema Nabii Musa na hata YESU KRISTO walikunywa maji kutoka Tanzania maana tumefundishwa uhai wa nchi ya MISRI unatokana na mto Nile (Nile is Egypt and Egypt is Nile). Shughuli zote za kilimo na maisha za wakazi wa Misri zinategemea mto Nile unaotoa maji yake Ziwa Victoria.
Ukitaka kusimama sehemu yenye mwinuko mrefu kuliko zote barani Afrika ili kujionea uzuri wa bara zima inakulazimu uje Tanzania kisha upande mlima Kilimanjaro. Aidha, ukitaka kuzama sehemu yenye kina kirefu kwenda chini barani Afrika inakulazimu tena uje Tanzania katika ziwa Tanganyika. Ndilo ziwa lenye kina kirefu kuliko yote Afrika na la pili duniani. Hata mti mrefu kuliko yote barani Afrika uko nchini Tanzania. Una urefu wa mita 81, unatoka katika familia ya Entandrophragma excelsum (Mti mrefu zaidi Afrika wagunduliwa Tanzania - BBC News Swahili).
Ni katika taifa la Tanzania pekee unaweza kukutana na aina mbalimbali za wanyama na viumbe wa asili. Tuna aina za vyura ambao mataifa mengine duniani hayana. Vyura aina ya Nectophrynoides asperginis (Vyura wa kihansi), hawapatikani sehemu nyingine yoyote duniani isipokuwa katika bonde la Kihansi nchini Tanzania. Tanzania ni miongoni mwa nchi 6 za maziwa makuu barani Afrika zikiwa na jumla ya maziwa 4 (Viktoria, Tanganyika, Nyasa na Rukwa) kati ya maziwa 9 (tisa) yaliyoko katika orodha rasmi ya maziwa makuu. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 10 ya aina zote za samaki duniani zinapatikana katika maziwa haya makuu huku maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa yakichangia moja ya nne (1/4) ya maji baridi yanayopatinana duniani.
Taifa hili ambalo ni la 13 kwa ukubwa wa eneo barani Afrika na la 31 duniani, limetenga zaidi ya asilimia 35 ya ardhi yote kuwa hifadhi ya taifa kwa maana ya mapori ya akiba na mbuga za wanyama. Kwa zaidi ya nusu karne sasa tumekuwa kisiwa cha Amani na kimbilio la wanyonge kutoka mataifa mbalimbali.
Pamoja na taifa hili kuwa na makabila zaidi ya 120 na tofauti mbalimbali za kiimani, bado tumeendelea kuishangaza dunia kwa jinsi tunavyoishi kwa kuvumiliana na kuelewana. Ni taifa pekee Afrika ambalo licha ya watu wake kuwa na lugha zao nyingi za asili, WOTE wanaunganishwa na lugha moja ya Kiswahili ambayo sio lugha ya mkoloni!
Tanzania imebarikiwa kuwa nchi ya pili barani Afrika kwa wingi wa mifugo (ng’ombe, mbuzi na kondoo) nyuma ya Ethiopia lakini hatuna bomba hata moja linalotiririsha maziwa. Bado Tanzania ni taifa linaloongoza kwa kuagiza maziwa ya kopo kutoka ughaibuni. Viatu, mikoba na bidhaa mbalimbali za ngozi ambazo taifa lingeweza kuzalisha hazipo tena kwa sababu tunaongoza kwa kuuza mifugo hai nchini Kenya kisha wao wanachinja na kuuza kupata bidhaa zaidi ya kumi. Watanzania tubadilike.
Tanzania imebarikiwa kuwa na misitu mingi ya asili pamoja na nyika. Ardhi nzuri tuliyonayo na mvua ya kutosha ni fursa nzuri ya kuwa na misitu mingi ya kupandwa nchini lakini haipo na wala hatuna bomba hata moja linalotiririsha asali katika misitu na nyika hizo! Mungu atupe nini?
Tanzania imebarikiwa kuwa na tambarare na mabonde mazuri kuliko mataifa mengi hapa duniani. Tuna bonde la mto Pangani lenye ukubwa wa kilometa za mraba 53,600 (Ukubwa sawa na mataifa ya Rwanda na Burundi kwa pamoja!), tuna bonde la mto Ruvuma lenye ukubwa wa kilometa za mraba 152,200 ambazo kati ya hizo kilometa za mraba 52,200 (ukubwa zaidi ya taifa la Denmark!) ziko nchini Tanzania na eneo linalosalia liko Msumbiji na Malawi.
Tuna bonde la ziwa Nyasa lenye kilometa za mraba 132,000 lililoko katika nchi za Tanzania, Malawi na Msumbiji ambapo eneo la bonde kwa Tanzania ni kilometa za mraba 37,000 (ukubwa zaidi ya taifa la Ubelgiji!). Tuna bonde la ziwa Rukwa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 88,000 (ukubwa zaidi ya taifa la Austria). Pia tuna bonde la Wami Ruvu lenye kilometa za mraba 72,930 (ukubwa mara mbili ya mataifa ya Haiti na Jamaica kwa pamoja!). Pia tunayo mabonde ya ziwa Tanganyika, bonde la Ziwa Viktoria na mabonde ya ziwa Eyasi, Manyara na Bubu. Mabonde yote haya yana maji ya kutosha na ardhi yenye rutuba kwa kilimo na ufugaji wa kisasa wa samaki.
Katika utajiri wa maliasili ni wazi taifa letu limependelewa. Mpaka sasa tuna akiba ya madini ya Dhahabu inayofikia wakia milioni 36, uzalishaji utakaotufanya tushike nafasi ya tatu baada ya Ghana na Afrika Kusini. Tuna hazina kubwa ya madini ya Urani, uzalishaji ambao utatuweka katika nafasi ya tatu Afrika baada ya Niger na Namibia. Tuna gesi asilia yenye ujazo wa zaidi ya futi trilioni 26, tuna madini ya makaa ya mawe yanayofikia tani milioni 50.94, tuna madini ya chuma pia. Tuna madini adimu ya Tanzanite ambayo hayapatikani sehemu yoyote ile duniani na zaidi ya yote, hivi karibuni imepatikana hazina kubwa ya madini ya magadi soda huko Monduli mkoani Arusha.
Eneo hilo lenye mita za ujazo bilioni 4.6 za madini hayo zitaipaisha Tanzania hadi nafasi ya tatu nyuma ya Marekani na Uturuki kwa uzalishaji. Pamoja na hazina yote hii, bado tunaambiwa kwa mdomo eti pale jangwani upande wa pili wa Misri ndipo ilipokuwa bustani ya Edeni. NAKATAA.
Kitabu kitakatifu cha Biblia kinaielezea bustani ile kuwa ilizungukwa na maji pande zote nne kwa maana ya kaskazini, kusini, mashariki na magharibi na maji yale yalikuwa yakitiririka kuingia bustanini (Mwanzo 2:10-14). Hakuna TAIFA lingine hapa duniani lenye aina hiyo ya maji zaidi ya Tanzania. Upande wa kaskazini tumezungukwa na mito ya maji ya ziwa Viktoria, hili ni ziwa la kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la pili duniani baada ya ziwa Superior lililoko Amerika ya Kaskazini.
Upande wa Magharibi tumezungukwa na ziwa Tanganyika ambalo ni ziwa lenye kina kirefu kuliko yote barani Afrika na la pili duniani baada ya ziwa Baikal lililoko Asia. Upande wa Kusini tumezungukwa na ziwa Nyasa. Hili ni ziwa la tisa kwa ukubwa duniani, la tatu kwa ukubwa na la pili kwa kina barani Afrika. Upande wa mashariki tumezungukwa na ufukwe wa Bahari ya Hindi wenye urefu wa zaidi ya kilomita 800 kuanzia mkoani Tanga hadi Mtwara. Pamoja na maji yote haya yanayotiririshwa na Mungu kuingia bustanini bado mnaniambia hii sio Edeni? POA NIKOSOENI LAKINI EDENI HAIKO MASHARIKI YA KATI.
Watanzania tuamke, tubadilike na tupambane katika kuinua uchumi wa taifa letu. Wasomi tuache kunung’unika na badala yake tujikite katika kupambana na changamoto zinazoikumba jamii kwa kuzibadili kuwa fusa za ajira na serikali ijikite katika kutengeneza mazingira bora na yaliyo rafiki kwa raia wake kuishi kwa amani na utulivu. (gnyaissa@yahoo.com)

Upvote
3