Baba Mkali
JF-Expert Member
- Feb 9, 2011
- 810
- 813
Umeelezea vizuri, ila ball boys itabidi nichunguze tena, wale ma
Kama wapo basi nakuaga bize sana kuangalia matukio ya ndani ya uwanja, cha msingi hilo sio swali alilouliza mleta mada, mpe jibu analotaka!
Imenibidi nigoogle kidogo hii habari kwani ilinishika hamaniko!!!
Nimepata maelezo ya kiasi. Nitayaeleza kwa kifupi. Matamanio ya soka (kwa epl) ni kuona mpira mmoja tu unatumika dakika zote tisini za mchezo ili kuondoa uwezekano wa kudanganya; mfano: ikiwa ruhusa muda wowote kuingiza mpira mwingine, je itakuwaje "ballboy" akiingiza mpira wa pili wakati wa kwanza haujatoka kabisa (completely) na mshambuliaji akautumia huo kutoa pasi ya kufunga ilihal mabeki wameshaokoa mpira wa awali?....ni jambo gumu kutokea ila laweza kutokea. Andiko hilo limetoa mifano mingine michache. Wanachofanya ni kuhakikisha mpira mmoja tu ndio unatumika kadiri ya inavyowezekana (Mpira ukitoka usubiriwe hadi urudishwe uwanjani) ila kwa wakati mwingi ni vigumu kutumia mpira mmoja. Moja ya athari za kutumia mpira mmoja ni kuongezwa muda mwingi wa nyongeza (extra time).
... kwa maelezo hayo inawezekana barafuyamoto uko sahihi kwenye jibu lako la awali!!