Niliamua kukunja jamvi - Ndoto ya Machimbo.com

Niliamua kukunja jamvi - Ndoto ya Machimbo.com

Samedi Amba

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2018
Posts
227
Reaction score
178
Habari wanajamvi,

Natumaini kuwa mnaendelea vizuri. Moja kwa moja kwenye mada...

Nakumbuka nilikuja kwenu na wazo majuzi. Nilitamani kutengeneza mfumo utakao wawezesha wateja kununua kwa bei ndogo na wauzaji kuwafikia wanunuzi moja kwa moja.

Nikiwa "chini ya maji", nilipitia phases kadhaa, kujaribu kuwafikia wauzaji kwa ajili ya kufanya ubia nao, as well as kufanya price research.

Changamoto kubwa nlokutana nazo ni hizi:
  1. Wauzaji wengi walishirikiana na mimi na kunipa data zao. Ilikuwa rahisi kujua majina yao, mtaa wanakopatikana, na bidhaa wanazouza, in general.
  2. Shida ilianza pale ambapo nilianza kuchimba na kutaka kufahamu details za bidhaa moja moja (maana machimbo.com ilipaswa kuwa "product first", maana yake ni kuwa tulitaka kulenga bidhaa kwanza, siyo machimbo merely). Wauzaji wengi waliona kazi kunipa details zao, hata pamoja na ukweli kwamba nilikuwa na nia nzuri tu ya kuwasaidia kuconnect na wateja.
  3. Jambo ambalo liliniuma kichwa nkaona itakuwa mtihani, ni jinsi ya kucharge. Kuna model niliweka, lakini naona ilinipa changamoto kabla sijaanza.
Kama kuna mtu ambaye angetamani kutengeneza kitu kama nilichokifanya mimi (origial thread hii hapa: Machimbo ya Kariakoo Mkononi Mwako), au tayari anayo, tuonane tushare mawili, matatu na nkupe data nilizokusanya, kwa ajili ya wewe kuendelea.

Overally, nimejifunza mengi, na yote haya yananibeba ninapolenga product nyingine ya kesho.

Nashukuru sana wanaJF walionitia moyo, walionichallenge, na walionikumbusha kuwa kuna ushindani kwenye chochote nnachopanga kukifanya.
 
Back
Top Bottom