Nilichoelewa ndege zetu Gharama yake ni Trilion 1.28 tu

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2017
Posts
415
Reaction score
361
Nilicho elewa ndege zetu Gharama yake ni Trilion 1.28 tu

Ukiigawanya hiyo pesa kwa Watanzania milioni 60

Trillion 1.28 ÷ milioni 60

1,280,000,000,000 ÷ 60,000,000 = 21333

Kila mtanzania atapata elfu 21.

Sasa kazi kwenu mziuze ndege zetu au mtafute bodi ya wakurugenzi yenye wataalamu wa mambo ya usafiri wa anga ili washauriane jinsi ya kuendesha kampuni ili ipate faida?

Ama mrekibishe hiyo sheria ya kuwakodishia ndege ATCL hata kupindi cha majanga ambayo ndege haziruhusiwi kuruka?

Ama mrekebishe viwanja vya ndege ili viruhusu ndege kutua mchana na usiku pamoja na kutua zikiwa zimepakia abiria siti zote.

Sasa maamuzi yamo kwenu, ila hiyo Trilioni 1.28 hata mishahara ya miezi miwili tu sina hakika kama itaweza kulipa.

Ushauri wangu.
Serikali mkishindwa kufanya hiyo biashara mtakua mmeonyesha uzaifu mkubwa. Hapo kinachotakiwa hiyo biashara endeleeni kuifanya, fuateni ushauri mliopewa na CAG, msifuate ushauri wa wabunge wala watu wa mitandaoni.
 
Watu wajinga walijingishwa na aliyekuwa mjinga wa taifa wakajazwq pale airport na kusifia wakiaminishwa kwamba yale yalikuwa maendleo haya sasa waje wasifie hapa.

Nchi ina wajinga kibao hii.
 
Kwa hiyo hata bi mkubwa naye ni mjinga,maana naye alikuwepo!
 
Watu wajinga walijingishwa na aliyekuwa mjinga wa taifa wakajazwq pale airport na kusifia wakiaminishwa kwamba yale yalikuwa maendleo haya sasa waje wasifie hapa.

Nchi ina wajinga kibao hii.
wewe unaongelea ujinga gani mkuu, acha kutukana watu, au nawewe unawaza kuuza ndege zetu.
 
Changanya na hayo mahasara yake halafu kaa chini tafakari hizo fedha zingepelekwa hata kwenye Elimu Kilimo na Mikopo yenye riba nafuu

Kwenye ruzuku ya vifaa vya ujenzi
Bado ni pesa ndogo isingetosha nimekokotoa pale juu. Ni pesa ndogo sana hiyo Ukilinganisha na idadi ya watanzania.
 
Ndege wangenunua chache mbili hivi ningewaelewa lundo la ndege wakati mifumo ya biashara ipo kimafia ndege ikienda njia ya SA anatafutwa anaewadai kukamata ndege zenu ili wanaopata waendelee kupata kama tumeshindwa biashara ya korosho tutaweza usafirishaji wa anga kwa muda mfupi kweli...
 
BwaMleta uzi kapigwa hadi Ban nini kilichomsibu
 
Nilicho elewa ndege zetu Gharama yake ni Trilion 1.28 tu

Ukiigawanya hiyo pesa kwa Watanzania milioni 60

Trillion 1.28 ÷ milioni 60

1,280,000,000,000 ÷ 60,000,000 = 21333

Kila mtanzania atapata elfu 21.

Sasa kazi kwenu mziuze ndege zetu au mtafute bodi ya wakurugenzi yenye wataalamu wa mambo ya usafiri wa anga ili washauriane jinsi ya kuendesha kampuni ili ipate faida?

Ama mrekibishe hiyo sheria ya kuwakodishia ndege ATCL hata kupindi cha majanga ambayo ndege haziruhusiwi kuruka?

Ama mrekebishe viwanja vya ndege ili viruhusu ndege kutua mchana na usiku pamoja na kutua zikiwa zimepakia abiria siti zote.

Sasa maamuzi yamo kwenu, ila hiyo Trilioni 1.28 hata mishahara ya miezi miwili tu sina hakika kama itaweza kulipa.

Ushauri wangu.
Serikali mkishindwa kufanya hiyo biashara mtakua mmeonyesha uzaifu mkubwa. Hapo kinachotakiwa hiyo biashara endeleeni kuifanya, fuateni ushauri mliopewa na CAG, msifuate ushauri wa wabunge wala watu wa mitandaoni.
Kupata hasara kwa makampuni ya ndege katika msimu huu wa covid haiepukiki kwa sababu ndege hazifanyi kazi lakini gharama za wafanyakazi lazima ulipe pia kuendelea kuzitunza ndege ni gharama sana. Mashirika yote duniani yamerekodi hasara kwa msimu wa mwaka 2020. Na pengine hasara hiyo itaendelea kuwepo tu mpaka hali ya covid itapokuwa sawa na safari kurejea kama awali.
JPM bado ni shujaa, hasa kwa kununua ndege kwa fedha Taslimu. Ingekuwa ni mkopo wadai wangekuwa wanahesabu riba tu.
Magufuli was visionary, he fore sight. Ndege ni rasilimali muhimu sana katika uchumi hata kama haizalishi faida. Ni mojawapo ya alama ya nguvu kwa taifa.
 
Hashimu lwenje,

..trillion 1.28 tuwape MABEBERU wanaotengeneza ndege?

..au trillion 1.28 tuwape WANANCHI ziingie ktm mzunguko wa matumizi hapa nchini.

..kati ya choice hizo mbili unadhani ipi ina manufaa kwa Watz?

NB:

..1.28 trillion zinatosha kujenga madaraja mawili yenye ukubwa unaolingana na daraja la Kigongo--Busisi.
 
Kupata hasara kwa makampuni ya ndege katika msimu huu wa covid haiepukiki kwa sababu ndege hazifanyi kazi lakini gharama za wafanyakazi lazima ulipe pia kuendelea kuzitunza ndege ni gharama sana. Mashirika yote duniani yamerekodi hasara kwa msimu wa mwaka 2020. Na pengine hasara hiyo itaendelea kuwepo tu mpaka hali ya covid itapokuwa sawa na safari kurejea kama awali.
JPM bado ni shujaa, hasa kwa kununua ndege kwa fedha Taslimu. Ingekuwa ni mkopo wadai wangekuwa wanahesabu riba tu.
Magufuli was visionary, he fore sight. Ndege ni rasilimali muhimu sana katika uchumi hata kama haizalishi faida. Ni mojawapo ya alama ya nguvu kwa taifa.

..Atcl ilikuwa inaendeshwa kwa hasara kabla mlipuko wa ugonjwa wa corona.

..Pia sio kweli kwamba ndege ni alama ya nguvu ya taifa.

..Marekani hawana shirika la ndege la serikali. Tanzania tuna shirika la ndege la serikali. Je, Tanzania tuna nguvu kuliko Marekani?

..Magufuli angekuwa visionary angejihadhari na biashara ya usafiri wa anga. Ni biashara ambayo uwezekano wa kupata HASARA uko wazi bila kificho.
 
Back
Top Bottom