Nilichogundua watu wanaodharaulika mitaani ndo wanaopendwa

Nilichogundua watu wanaodharaulika mitaani ndo wanaopendwa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Sote tunaishi mitaani tumeshakutana na kauli kuwa Fulani hajiheshimu anadharaulika kwa sababu labda ya pombe au Fulani anaongea sana au Fulani anatukana sana hivyo jamii haimpi heshima.

Kwa utafiti mdogo nilioufanya nimegundua wenye vimatendo hivyo vya ajabu ndo wanaopendwa zaidi na watu,hawasengenywi na pia wanasaidiwa sana kuliko wale wanaonekana wana tabia nzuri za ukimya ukimya kutojichanganya na watu.

Kwa mfano mtu mlevimlevi ambaye sio mgomvi anaaminika mtaani hata akiwa na shida ya chakula wanampa na hawatamsimanga wala kumsema vibaya ila Yule wa matawi ya juu ikitokea kaomba kitu lazima wamdiscuss.

Natumaini nimeeleweka kidogo Nihitimishe kwa kusema kujichanganya ni muhimu sana kuliko kujitenga hasara zake ni mambo yako yatafahamika mpaka yatachokwa ukitoa boko wanaona sawa na kwenye mkao ukikosekana pengo lako linaonekana hawachelewi kukutafuta ujumuike nao yaani kwao unakuwa kama mtu unayekamilisha amani mkaoni.
 
Dar es salaam watu wana macho mekundu utadhani wamevuta bhangeeee..
 
Back
Top Bottom