Nilichojifunza dakika chache baada ya kumaliza chuo: Kujilipua na Kujihatarisha (risk taking) kutakusaidia kutoboa mapema kuliko kusubiri utaratibu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Niliingia first Year nikiona mwaka wa mwisho wote wanaijiwa na waajili wakaanze kazi. Siku namaliza hakuna hata hata mmoja aliyekuja. Hali ilikuwa imebadilika. Nilikuwa nimeshaapa sirudi nyumbani afe kipa afe beki.

Plan B
Niliandaa barua na CV kama 200 hivi. Za elimu zote, form 4, six, ya chuo na ya general degree. Nikapuyanga kila ofisi niliyoigugo posta. Lengo sio ajira lengo ni kuzuia njaa kwanza wakati mengine yatafuata hukohuko. Nikatoka kapa, nikaishia kumaliza sole za viatu tu.

Plan C
Nilikutana na mbabe mmoja aliyenipa mbinu ya kuforce kuajiliwa. Huyu alisoma Ulaya, akasota bongo hadi alipojilipua. Kuforce kukutana na bosi wa makampuni kwa kukwepa viunzi vya machawa na Makatibu Muhtasi wanaomzunguka.

Nikaforce ofisi moja, nilimrubuni secretary akanipa access ya kuonana na Boss. Yule jamaa ni mtu mwema sana. Wakubwa wengi ni watu wema na wasikivu sana. Nilivyojieleza na kutestiwa kidogo kesho yake nikaingia kitengo.

Hakuna Interview, hakuna pepa, hiyo transition ilinivusha hadi nilipoendelea na mission zangu ambazo ndio zilikuwa kipaumbele changu.

Kama mkristo nimejifunza.

Sio kila kitu utakipata kwa kufuata utaratibu. Taratibu nyingi na sheria na miongozo ni kwa ajili ya watu wasio na connection.

Nilijifunza, lazima ujilipua na kujihatarisha ili mambo yaende. Sio kila kitu utakipata kwa kusubiri utaratibu. Ukiomba Mungu akikupa kibali unaingia popote kama Malkia Ester alivyowaokoa wayahudi kwa kuingia kwa mfalme kinyume na utaratibu.

Sijasema ni lini, wapi, maana msingi ni nilichojifunza. Hadi leo nikitaka chochote kwa yeyote bila kujali cheo au hadhi nitatafuta mbinu zote nimfikie kama wale jamaa waliotoboa bati ili mgonjwa wao amfikie Yesu baada ya kuona njia za kawaida zimezibwa na makutano.

Ni hayo tu.
 
Nimekumbuka mbali sana. Aisee, njaa inaweza kukufanya ujaribu mambo ambayo kikawaida ukiwa umeridhika usingeweza kufanya.

I used to live in this fact, there is always a success point that everyone will have their way through once/more in a lifetime. It's only a matter of time!
 
Hii njia imenisaidia sana,nilichojifunza binadamu watakukatisha tamaa sana na kukuzibia njia,pambana uonane na mkuu wa taaisis husika sio hawa subordinates au machawa watakusumbua sana na kukuwekea vikwazo vingi na vitisho juuu.
 
Ungeelezea jinsi ya kupata connections maana ofisi nyingine ukiforce utaonekana kichaa
Hakuna jinsi mkuu. Nilijitoa muhanga kwenda jengo moja liko opposite na iliyokuwa Sheraton hotel. Nikaforce kuonana na bosi. Huwezi kuonekana kichaa kama umependeza na unajua kuongea vizuri. Hata hivyo ukitaka usionekane kichaa utasubiri sana.
 
Hii njia imenisaidia sana,nilichojifunza binadamu watakukatisha tamaa sana na kukuzibia njia,pambana uonane na mkuu wa taaisis husika sio hawa subordinates au machawa watakusumbua sana na kukuwekea vikwazo vingi na vitisho juuu.
Safi sana mkuu.
 
Madini adhimu haya...

Nimejifunza hapa.
Ni kweli. Sisi wakristo tunajifunza Yesu alijishusha akaonekana kama lofa tu ili afikie malengo. Watu walimuona mzinzi, mnywa gongo, mchawi, wengine msalabani walijua Mungu ndiye anamuadhibu, ila kikubwa yeye alijijua ni nani hivyo hayo hayakumpa shida.

Ni matumizi mabaya ya nishati za maisha kutaka ueleweke. Kama unajielewa na unajua unataka nini watu waache wachague watakavyokuona.
Funzo la kwanza kwenye maisha nililojifunza ni kuidharau aibu.
 
Japokuwa siamini kwenye habari za uwepo wa Yesu na Mungu.

Naheshimu mawazo yako pia ya huu uzi.
Ni matumizi mabaya ya nishati za maisha kutaka ueleweke. Kama unajielewa na unajua unataka nini watu waache wachague watakavyokuona.
Funzo la kwanza kwenye maisha nililojifunza ni kuidharau aibu.
Yeah! Absolutely yes.

Umenena.
 
Ungeelezea jinsi ya kupata connections maana ofisi nyingine ukiforce utaonekana kichaa
Hahahahah huforce kwa kupiga kelele,
Unatafuta connection eg, unamuhonga secretary akupe ratiba ya boss uone ni wapi unaweza kutana nae, eg bar yake au hata akusaidie, kuweka appointment nae katika free time yake
 
Niliingia first Year nikiona mwaka wa mwisho wote wanaijiwa na waajili wakaanze kazi. Siku namaliza hakuna hata hata mmoja aliyekuja. Hali ilikuwa imebadilika. Nilikuwa nimeshaapa sirudi nyumbani afe kipa afe beki.

Plan B
Niliandaa barua na CV kama 200 hivi. Za elimu zote, form 4, six, ya chuo na ya general degree. Nikapuyanga kila ofisi niliyoigugo posta. Lengo sio ajira lengo ni kuzuia njaa kwanza wakati mengine yatafuata hukohuko. Nikatoka kapa, nikaishia kumaliza sole za viatu tu.

Plan C
Nilikutana na mbabe mmoja aliyenipa mbinu ya kuforce kuajiliwa. Huyu alisoma Ulaya, akasota bongo hadi alipojilipua. Kuforce kukutana na bosi wa makampuni kwa kukwepa viunzi vya machawa na Makatibu Muhtasi wanaomzunguka.

Nikaforce ofisi moja, nilimrubuni secretary akanipa access ya kuonana na Boss. Yule jamaa ni mtu mwema sana. Wakubwa wengi ni watu wema na wasikivu sana. Nilivyojieleza na kutestiwa kidogo kesho yake nikaingia kitengo.

Hakuna Interview, hakuna pepa, hiyo transition ilinivusha hadi nilipoendelea na mission zangu ambazo ndio zilikuwa kipaumbele changu.

Kama mkristo nimejifunza.

Sio kila kitu utakipata kwa kufuata utaratibu. Taratibu nyingi na sheria na miongozo ni kwa ajili ya watu wasio na connection.

Nilijifunza, lazima ujilipua na kujihatarisha ili mambo yaende. Sio kila kitu utakipata kwa kusubiri utaratibu. Ukiomba Mungu akikupa kibali unaingia popote kama Malkia Ester alivyowaokoa wayahudi kwa kuingia kwa mfalme kinyume na utaratibu.

Sijasema ni lini, wapi, maana msingi ni nilichojifunza. Hadi leo nikitaka chochote kwa yeyote bila kujali cheo au hadhi nitatafuta mbinu zote nimfikie kama wale jamaa waliotoboa bati ili mgonjwa wao amfikie Yesu baada ya kuona njia za kawaida zimezibwa na makutano.

Ni hayo tu.
Kweli tupu.. Mafanikio kwenye nyanja yoyote ile yanataka watu tough na walio determine kuwa vile watakavyo haijalishi leo inawaambia nini.
 
Back
Top Bottom