Vicenza
JF-Expert Member
- Oct 5, 2019
- 1,020
- 1,515
Habari za saa wana Jf,
Jana majira ya saa moja usiku nilipanda daladala ya kwenda kwa moromboo,wenyeji wa arusha bac mtakuwa mnaelewa huu mtaa kwa sifa za matukio mengi ya wizi kwenye daladala na hata mtaani,na waathirika wengi wa haya matukio ni kina mama na wadada ndio wanakuwa wa hanga wakubwa kwenye haya matukio ya uporaji mtaani na wizi kwenye daladala.
Bac nirejee kwenye tukio nililoliona jana ambapo kulikuwa na mama mmoja alikuwa amekaa siti ya nyuma kabisa wengi wanapenda kuita ubalozini,kipindi mama huyu ameketi akiwa anasubiri safari yake imalizike salama kabisa bila shida yoyote ghafla mama huyo akamwambia konda asimamishe gari kwenye kituo anachoshukia,konda bila hiyana yoyote akatii kauli ya abiria wake na gari ikasimama,alivyoshuka huyo mama kabla gari halijaondoka akamwambia konda kwa sauti kubwa na nukuu "pale nyuma kuna mwizi".abiria wote wakaanza kunongo'na kwa chini kama hawajali,ikumbukwe kondaa huyo na dereva ni vijana wa around miaka 30s,bac konda na dereva wake wakamuambia yule mwizi ashuke chini wakati uo yule mama akiwa bado anaongea jinsi yule mwizi alivyokuwa anataka kumuibia kipochi chake lakin hakufanikiwa,yule mwizi akatii amri na kushuka chini akiwa anasubiriwa kwa matamanio makubwa na bodaboda kwenye kile kituo,alivyo chuka chini alika ribishwa na kichapo kikali na umati uliokuwa una msubiria chini ikiwemo bodaboda,dereva na kondakta,wakati yule mwizi anapata adhabu akajitokeza abiria mmoja alikuwa amekaa siti karibu na mlango wa daladala akiwa anajaribu kumtetea yule mwizi asipigwe,
Kwa kwel sikuamin macho yangu ,yule mzee alijikuta anageuziwa kichapo na kondakta na dereva kwa kupigwa vibao 6 bila kujua vimetoka wap,huku abiria wote wakistaajabu mzee alivyo tolewa mfano,ikumbukwe abiria na wao hasa kina mama walikuwa wana mtetea yule mwizi kwa kusema asipigwe,lakin kwa bahati mbaya yule mzee alijikuta akitoa sauti zaid
kuliko abiria wote na kutaka kushuka ili kumtetea yule mwizi,sasa pakawa na matukio mawili kwa wakati mmoja,
Kwa tukio hilo wakati mzee anapigwa makofi na ngumi na umati mchache akiwemo konda,dereva na bodaboda,akiwa anaambiwa "usijaribu kumtetea mwizi hata siku moja unaweza uka chomwa moto"bac yule mwizi akawa amesaulika na kuponyoka akiwa ameshachezea kipigo cha dakika chache wakati uo abiria wakiwa wanaogopa kuongea tena na kushuudia mzee wa watu ana chapwa makofi na vijana wadogo wakiwa wanasema kwa nn ana mtetea mwizi au anamjua?.roho iliniuma ila sikuweza fanya chochote kuhofia kuwekwa mfano kwa kujaribu kutetea yule mzee asipigwe,
Kwa kuelezea kidogo konda alikuwa na hasira mbaya sana akiwa anatoa mate mdomon na kumshika yule mzee shati akiwa anampiga ila mwishowe mzee aka achiwa akiwa bado ndan ya gari,bac safari ikaendelea ila bado abiria walikuwa wanaongea tukio la yule mwizi na yule mzee,wakati huo derava na konda wanasema "abiria wanalamikaga wanaibiwa ndani ya daladala wakisema konda na dereva ndio wanashirikiana na wezi kuiba ila wezi wakikamatwa abiria wana watetea tena".ila nilichokiona kwa huyo konda na dereva walikuwa ni watu wa tofauti waki pambana kutoa adhabu kwa mwizi bila kuchelewa.safari ya mzee wa watu ikafika tamati na kushuka kimya bila kuongea na mtu akiwa na upole wa hali ya juu.
Mwisho: wale wote wanaokuja arusha wawe makini sana na haya maeneo hasa usiku
-1.Moromboo
-2.Ungalimited
-3Olasiti
#pole sana mzee kwa yale makofi inasikitisha sana vijana wadogo wanampiga mzee wa miaka around 50s kwa kujaribu kumtetea mwizi ndani ya daladala.