Nilichokiona jana kwenye daladala ya kwa Morombo-Arusha

Chunga sana kutembea usiku maeneo ambayo wewe sio mwenyeji. Pia kuwa makini sana ikishafika usiku hiyo njia kuanzia Kilombero mpaka mbele kidogo ya Soko Mjinga (Embassy Garage) hiyo njia hapo ina wahuni wa Ngarenaro ukijichanganya tu hata ukiwa kwenye gari unapigwa tukio fresh tu.

Nimekaa sana hapo Back Town (Ngarenaro) watu wanapigwa matukio hata mchana kweupe kwenye magari yani kibaka anakuwa kama anavuka road ukiwe kioo kipo wazi na unachat au unaongea na simu inatembea au hata pochi. Na ubaya wa hapo Ngarenaro mpaka Soko Mjinga yani ukivula tu lami upande wa chini hatua tano ushaingia vichocho so mwizi akikwapua tu hatua tano humuoni ni machocho yakufa mtu huko huingii kama sio mwenyeji hata kama ni mchana.

Usiku ukipita kwa mguu imekula kwako. Ukipata breakdown hayo maeneo imekula. Machalii wa Matejoo na Ngarna ndio kituo chao cha kazi hiyo road kuanzia mida ya saa moja usiku.

Kuhusu wizi kwenye vi hiace (vifodi) au coaster (baadhi ya sehemu zipo coaster) hilo sio kwa Morombo tu au Olasiti kama ulivyosema mleta mada. Hilo ni suala la nchi nzima popote pale ukikaa kiree hasa kwenye haya mausafiri ya kunabanana lazima wahuni wakuoshe.
 
Mjini kama jambo halikuhusu bora upotezee tu hata kama unaona upande fulani unakosea.....unaweza jikuta unaathirika tu bila sababu......nakujikuta unapotezewa muda bure
 
Tengeru kunaitwa kwa mafundi simu
 
Hata Warioba alipigwa na Makonda! Si ni life tu
 
Kilichoniuma ni mzee kupigwa makofi na konda bila kuangalia umri wake
Bila shaka hujawahi kuibiwa na huyajui maumivu yake.

Siku ukiibiwa ndio utaelewa kwanini mzee aligeuziwa vibao na mwizi akaachwa na kusepa
 
Wewe kwa maoni yako unaonaje huyo chalii aliyechezea kichapo ana sura ya wizi wizi??
alikuwa anaonekana mwizi kwa maana abiria walokuwa wamekaa na yy walihic anachokonoa mkoba wa mama pemben
 
Bila shaka hujawahi kuibiwa na huyajui maumivu yake.

Siku ukiibiwa ndio utaelewa kwanini mzee aligeuziwa vibao na mwizi akaachwa na kusepa
nilishaibiwa ,ila tu mzee alionewa na vijana wadogo
 
Hao vibaka wa arusha ni wazembe sana uwa wanajifanya nao ni abiria wakishaiba ndani ya hiace wanashukia njiani, mi kuna kipindi 2018 nilipanda nao kwa mrombo-kilombero wakanipiga tecno y3 yangu wakataka kushukia corner ya mbauda nikastuka kucheck kwenye kibag sina simu nilishuka nao wakatoa simu😂😂wengine pia wanafahamiana na drivers na kondactors.
 
Mkiambiwa Mjini Muache Shobo Ndo Muelewe,Miaka ya 2010 Ubungo Nakatiza Zangu Ilikuwa Jumapili Saa 10-11 Hivi,Nkakuta Umati Wanaangalia Ule Mchezo Wa Karata,Kipindi Hio Machinga Kibao Pembezoni Mwa Barabara,Kidume Nkajisogeza Nione Watu Wanavyoliwa,Sasa Kukawa na Mama Mmoja Nae Akavutiwa Kuucheza Ule Mchezo,Karata Zikazungushwa Kama Kawaida Yao,Wa Nje Unaona Kabisa Hapa Kaliwa Au Kala,Mama Akakosea Si Nikashoboka Kumbonyeza Aweke Hela Kwenye Kula,Nilikula Vibao Viwili,Haki Ya Nani Sikuona Kilipotokea,Yani Hadi Leo Najiuliza Nani Alinipigaga,Niliondoka Hilo Eneo Kama Ambulance Hata Sikugeuka Nyuma,Nilijifunza Mipango ya Watu Ukiiona Iache Kama Ilivyo.

SHOBO Ukiwa Mjini Jizuie,Utaaibika 😁
 
Daa nimecheka sana utadhani mazuri, mjini kuna mambo aisee.
 
Sijawahi kuikubali Arusha kwa lolote lile, panaboa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…