Nilichokiona kwa rafiki yangu mwenye dada mgonjwa wa akili. Ni mtihani mzito kusema kweli

Nilichokiona kwa rafiki yangu mwenye dada mgonjwa wa akili. Ni mtihani mzito kusema kweli

Ruble

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
845
Reaction score
1,579
Miaka kadhaa nyuma nilipata kuishi kwenye familia ya rafiki yangu mkazi wa Dar es salaam. Rafiki yangu huyo kwa miaka yote toka tumefahamiana alikua amenieleza ana dada yake mkubwa (kwa sasa ana miaka 40+ dada yake) mwenye matatizo ya akili. Sikua nimewahi kumuona mpaka nilipoishi kwa wiki nzima pale kwao.

Nilishuhudia hisia mseto zs masikitiko na hasira ya wazi ya rafiki yangu juu ya mwenendo na tabia za dada yake.

Kuna mtu amewahi kua na ndugu mwenye shida ya akili tubadilishane visa na mikasa yao.

Kwa niliyoyaona pale. Hakika kuna watu wana mitihani.

1. Kuna siku jamaa akanieleza nusura nyumba yao iungue moto. Dada yake aliinjika sufuria ya maji kwenye gesi. Kukosa kutokea jirani kufika nyumbani kwao hadithi ingekua tofauti. Yule jirani alipofika tu akasikia harufu kali ya gesi ndio haraka akaingia ndani na kuzima.

2. Nyumba yao haiishi wageni. Kukiwa na wageni inamlazimu jamaa au mama yake muda wote kua alert na usafi wa chooni. Nakumbuka ilikua akiingia chooni basi kinachofuata wewe utayeingia lazima ufanye usafi ndio upatumie, kwa mwenye kinyaa hawezi.

3. Ni jeuri huyo na mbishi aisee kama una hasira unaweza kuua. Kwa muda niliokaa pale ilikua karibu kila siku atie hasara ama avunje chombo, au chochote kila mradi hasara.

4. Dada yake hua ana kawaida ya kwenda kuzurura na kurudi usiku wa saa 5 huko na kuendelea. Siku hiyo jamaa alimtandika na kumlaza nje. Haikusaidia kitu na bado akawa anaendelea kurudi usiku.

5. Huwa wana kawaida ya kumtuma kwa kumuandikia vitu. Maana hajui kusoma. Sasa siku hiyo katumwa vitu vya kupika na kulikua na wageni anasisitizwa mara mbilimbili awahi kurudi. Bwana akarudi saa 8 mchana na vitu. Aisee jamaa yangu alilalamika.

6. Dada yake anapenda kula bwana. Siku hiyo nyama ya fileti nusu kilo wameigandisha kwenye friji mboga ya kesho. Asubuhi kutahamaki mboga imeliwa yote. Akiulizwa anakaa kimya. Jamaa yangu alitaka kumpiga mama mzazi na mimi ikabidi tuingilie.
 
Usiombe yakukute yasikie tu wengine, nilikaa na kaka yangu kwa takribani wiki moja alipata changamoto ya akili, aisee alikua anaamka usiku ananza kuzunguka ndani qnafungua mlango atoke nje usiku anajipisha story mwenyewe, alafu mbabe sasa mwli jumba, nilikua na mdogo wangu jamaa akibadilika na kuleta ubabe dogo anajamba tu na kufungua mlango anatoka nje kwa uoga
 
Miaka kadhaa nyuma nilipata kuishi kwenye familia ya rafiki yangu mkazi wa Dar es salaam. Rafiki yangu huyo kwa miaka yote toka tumefahamiana alikua amenieleza ana dada yake mkubwa (kwa sasa ana miaka 40+ dada yake) mwenye matatizo ya akili. Sikua nimewahi kumuona mpaka nilipoishi kwa wiki nzima pale kwao.

Nilishuhudia hisia mseto zs masikitiko na hasira ya wazi ya rafiki yangu juu ya mwenendo na tabia za dada yake.

Kuna mtu amewahi kua na ndugu mwenye shida ya akili tubadilishane visa na mikasa yao.

Kwa niliyoyaona pale. Hakika kuna watu wana mitihani.
Hujatoa kisa hata kimoja mkuu, tunavutika vipi na huu uzi???​
 
Inaonekana huyu dada ni nunda tu sio kichaa huyo. Mgonjwa wa akili anaenda kuzurula anarudi mwenyewe home saa 5 usiku kila siku?
 
5. Huwa wana kawaida ya kumtuma kwa kumuandikia vitu. Maana hajui kusoma. Sasa siku hiyo katumwa vitu vya kupika na kulikua na wageni anasisitizwa mara mbilimbili awahi kurudi. Bwana akarudi saa 8 mchana na vitu. Aisee jamaa yangu alilalamika.
Hamko serious nyie
 
Inaonekana huyu dada ni nunda tu sio kichaa huyo. Mgonjwa wa akili anaenda kuzurula anarudi mwenyewe home saa 5 usiku kila siku?
Ana matatizo hata ukimuangalia unajua hazimo. Akiwa hasa anaongea. Kuzurura ni anakaa tu barabarani anashangaa watu. Kwa muda niliokaa pale akirudi anawarudia na matakataka ameokota huko. Makopo manyanya yaliyotupwa anawaletea.
 
Back
Top Bottom