Nilichokipenda baadaa ya kukisikia Kenya kuhusu Uchaguzi Mkuu 2022

Nilichokipenda baadaa ya kukisikia Kenya kuhusu Uchaguzi Mkuu 2022

Tibaiwa

Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
51
Reaction score
38
NILICHOKIPENDA BAADAA YA KUKISIKIA KENYA KUHUSU UCHAGUZI MKUU 2022.

Ukweli na uwazi pamoja na matumizi ya teknolojia (mtandao)
Duniani kote hakuna siasa safi inayoizidi hile ya ukweli na uwazi, hapa nchi Cambodia tumekuwa waumini wa maneno mazuri kuliko kuyaweka kwenye matendo.

Ukweli na uwazi ni maneno matamu yalitoka kwenye midomo ya mababu zetu na kuyanakishi kwenye vitabu hadi leo japo utamu huu niwakutamkika kuliko matendo.

NIMELISIKIAJE KENYA
Kupitia ripoti ya mwangalizi wa uchaguzi nilisikia akisema maneno yanayoimaanisha hivi ".....mawakala wa vyama vya siasa waliruhusiwa kuingia na simu janja na kuchukua picha za fomu za matokeo kwa kuwatumia wagombea wao/vyama vyao...". ninayoimani hata baada ya matokeo kutangazwa picha hizo bila kuhaririwa na waharifu wa masuala ya kimtandao ni kidhibitisho cha kumfanya mgombe akubali matokeo ya jumla kutoka kwenye tume ya uchaguzi au kupinga matokeo hayo kwa kupeleka nyaraka hizo kama ushaidi kwenye vyombo vyenye mamlaka husika sababu vilikuwa mstari wa mbele kumulika"Ukweli na uwazi".

HAPA NCHINI CAMBODIA TUJIFUNZE NINI KUTOKA KENYA.
Nguvu kubwa inayotumika kudai "katiba mpya" iwekezwe zaidi kwenye kuiweka kimatendo kauli tamu ya "ukweli na uwazi" kwa watu wote.

Kwani hata tume ikiwa huru lakini ikabaki na watu "waongo waongo" wasio simamia Ukweli na uwazi tutakuwa tumeondoa mlango kwa kuweka pazia. Na maanisha "kivuli cha katiba mpya ni tume huru"

Kaulimbiu ya zamani itasaidiwa na teknolojia kwa kuweka vitu wazi vya wasema ukweli.
#Ukweli na uwazi.
 

Attachments

  • Screenshot_20220823-191750.jpg
    Screenshot_20220823-191750.jpg
    62.6 KB · Views: 7
Back
Top Bottom