Mtumishi mimi sipo upande wa watesi nimejaribu ku share nilichokiona kwenye ulimwengu wa maono.
Hukuona sawasawa..
Kanuni ya Mungu Yehova, ni kuwa, akikupa ujumbe fulani kupitia aidha ndoto au maono ya namna yoyote, basi straight mpelekee muhusika as quick as you can within the time frame aliyokupa Mungu...
Wewe umetenda kinyume chake. Kwamba, umepewa ujumbe personal kwa ajili Tundu Lissu, lakini wewe unapita barabarani kumtangazia kila mtu (kuandika humu JF ni sawa na kuropoka hovyo huko barabarani)...
Na kwa sbb hii, ndoto na maono yako haya yanakosa sifa kuwa yametoka kwa Mungu Yehova bali ni hisia zako tu au unatumiwa na adui (ibilisi) kuleta confusions kwa kujua au bila wewe kujua...
However, hii haina maana kuwa Tundu Lissu hayuko ktk tishio la hawa hayawani wanaoiwinda yoho yake. Bado anaishi ktk tishio hili. Kila Mtanganyika anatambua hilo (wala hatuhitaji ndoto wala maono ya mtu yeyote)....
Aidha Tundu Lissu mwenyewe anajua na kutambua matishio hayo yote toka kwa watesi wake. Na kwa kuwa wote tunajua, usifikiri kuwa ulimwengu wa Roho umetulia. Watu kila kona ya nchi hii na duniani kote, wanapigana vita hii ya kiroho kumuombea Mtumishi wa Mungu huyu Ili Mungu amkumbatie na kumponya na kila hila na mikakati ya uovu ya hayawani hawa wa CCM na serikali yao haramu na dhalimu...
Tunaomba na tunaomba kwelikweli juu ya Tundu Lissu. Hatukuhitaji kusubiri hisia za watu wanazoziita ndoto au maono Ili kujua kuwa ndugu yetu yuko ktk hatari. Inajulikana miaka mingi iliyopita ndio maana hata zile risasi 16 za mwaka 2017 toka kwa hayawani hawahawa hazikutoa uhai wake. Ni kwa sbb, Munyu Yehova yu pamoja naye daima.. Amina🙏🙏🙏.
Imeandikwa👇
Ayubu 5:12-15 SUV
".....Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu, Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao. Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka. Wao hupatwa na giza wakati wa mchana, Hupapasa mchana vilevile kama usiku. Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari...."
Kupitia Neno hilo👆, Bwana Mungu Yehova asema hivi;
1. Mashauri (mashitaka yao ya uongo na udanganyifu sambamba na mikakati (strategies) za utekelezaji, yote yametanguliwa au yamebatilishwa!
2. Mikono yao na akili zao zimeshikwa na kufungwa ktk ulimwengu wa Roho na milele hawataweza kamwe kutimiza makusudi yao maovu!!
3. Kupitia hekima yao wenyewe ya kijinga na kipumbavu, wamenaswa ktk hila zao...!
4. Mashauri yao wanayoona ni ya kishupavu na kishujaa wakati ni uasi na uovu mtu mbele ya YESU KRISTO, yameshaharibika na kusambaratika haraka na muda mrefu!
5. Na kwa sababu hii, watapigwa upofu. Wakati wa mchana jua likiwa na nuru yake, wao wataona Giza na watatembea kwa kupapasa papasa..
6. Sisi na Tundu Lissu, Mungu Yehova keshatuokoa tayari toka katika makali ya panga zao (i.e bunduki, risasi, sumu zao na mbinu zao zote za uharibufu..)
👉Amka, tubu na Bwana Mungu ktk Yesu KRISTO atakurehemu
👉Mbingu na nchi na zishangilie na kuimba kwa furaha maana Bwana wa utukufu, Mungu wa miungu yote, Bwana wa mabwana wote, Mungu wa Majeshi yote amejitukuza na kujiinua ktk nchi na taifa tukufu la Tanganyika..!