Nilidhani marefa wanaopendelea ni wa Tanzania na NBC Yetu kumbe hata Ulaya? Goli la Netherlands lililokataliwa dhidi ya France lina Kosa gani?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kuanzia leo nitaacha rasmi Kuwalaumu Marefa wa Afrika kwa Kuvurunda kwa Kupendelea katika Ligi zetu na Mashindano yetu mbalimbali kwani kumbe huu Ugonjwa Sugu wa Marefa hauko tu Afrika na kwamba hata Ulaya kwa tunaowaamini nao uko?

Naomba kujua tatizo la Goli la Netherlands ambalo Kwangu Mimi GENTAMYCINE na kwa Utaalam wangu naona ni Goli halali kabisa. Sasa naanza kuamini kuwa Waamuzi wengi na wale walioko katika VAR huenda kweli wakawa ama Wanabeti au huwa na Chuki na Wachezaji fulani wa Timu Kubwa Kubwa.

Netherlands wameonewa na wamenyimwa Goli lao halali kabisa.
 
Offside ile yule mchezaji aliekua golini alihusika na mpira kwa kumziba kipa kuucheza mpira na pia alionekana kama anaukwepa mpira
Hivi Offside inakuweko katika Piga Nikupige kama ile? Kwahiyo Refarii alitaka yuko Mchezaji awe wapi ili asiwe Offside?
 
Offside ile yule mchezaji aliekua golini alihusika na mpira kwa kumziba kipa kuucheza mpira na pia alionekana kama anaukwepa mpira
Gapko alikua pembeni kabisa wala hakuwa usawa wa kipa halafu kipa alikua mbele yake kidogo
 
Unapokuwa kwenye offside position usifanye namna yoyote itakayopunguza ufanisi wa wachezaji wengine. Lile shuti makila kibao huyarukia na kuudaka au kuupangusa ila uwepo wa mchezaji wa timu pinzani umefanya kipa asiwe huru.
 
Uchambuzi wa Kimahaba na Chuki kwa Netherlands na Kuipendelea France kwakuwa ina Mbappe ambaye unampenda.
 
Kuanzia leo nitaacha rasmi Kuwalaumu Marefa wa Afrika kwa Kuvurunda kwa Kupendelea katika Ligi zetu na Mashindano yetu mbalimbali kwani kumbe huu Ugonjwa Sugu wa Marefa hauko tu Afrika na kwamba hata Ulaya kwa tunaowaamini nao uko?

Naomba kujua tatizo la Goli la Netherlands ambalo Kwangu Mimi GENTAMYCINE na kwa Utaalam wangu naona ni Goli halali kabisa. Sasa naanza kuamini kuwa Waamuzi wengi na wale walioko katika VAR huenda kweli wakawa ama Wanabeti au huwa na Chuki na Wachezaji fulani wa Timu Kubwa Kubwa.

Netherlands wameonewa na wamenyimwa Goli lao halali kabisa.
Ni wewe au mwingine!?
 
Kama hujaona kosa bora ushabikie rede tu mtalaam uchwara
Inashangaza sana. Mtu anaandika kuhusu michezo jukwaani na bado ile offside inamtatiza? Na bado anajiita mtaalamu. That was a clear offside. He interfered with play, by affecting the golie's mobility, visibility and accessibility.
 
Back
Top Bottom