Kalaga Baho Nongwa
JF-Expert Member
- Sep 27, 2020
- 9,953
- 23,150
Kwa niliyokutana nayo kalaga baho niseme tu safari ya maisha ni ndefu sna. Mikasa, visa na vibweka kwa akili za watanzania ndo mahala pake. Umaskini nao ndo umefika
Juzi wazee nilishikwa kwelikweli, maisha magumu sana Dira haioneshi wapi ni kaskazini. Basi nikajikoki kutafuta watu wazima kidogo wanipe neno la busara na maneno yanaleta hisia mpya na matumaini. Nikamcheki Shangazi yangu mmoja hiv akasema "njoo tujadili"
Basi wakuu kufika pale niko nje nimegonga hodi akauliza "nani?" Nikajibu "mm kalaga baho" nikasikia kawasha redio taarabu "siiina mda huooo , siiina! Wa kukaa vipembeni kudiskasi na mtu". Nikajua anatania
Kuingia ndani nimesalimia kukaa chini nikasikia karopoka "kula chuma hicho". Heeeh, kumbe mm wakati namueleza shida nije anishaur Ali furaha sana.
Nikaa chini ndugu zangu yule mama nilijuta!. Ushaur uliotoka pale ulisisitiza kujikaza kiume na maisha yakizid kuwa magum sana kanishauri nilie. Neno "ndo ukubwa huo! na ndo umekuwa uyaone ndo hayo!" Yalijirudia katika kila sentensi aliyoizungumza. Bas wakuu nikaona leo nimeyamunya nikajifanya napokea simu iliyoita nikatoka mpaka stendi nikakwea daladala nikarudi geto.
Kanipigia simu niko wapi mbona sijaaga. Nikamwambia nilipigiwa simu ya dharura sikutakiwa kubaki tuendelee na mazingumzo. Kama hakuwa na ushauri si angesema tu.
Yule mama mwehu nini?