Nilifanya bonge la sherehe baada ya mke wangu kufukuzwa kazi

Alvin A.

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2016
Posts
2,865
Reaction score
3,633
Huyu mke nilimuoa akiwa hana kitu, kwa bahati alitafutiwa kazi na ndugu yake kwenye kampuni moja ya simu akawa analipwa kama milioni 3 kwa mwezi fasheni na yeye yeye na fasheni vipodozi kila aina,handbag na nywele za laki mbili ndio mshahara wake ukawa unaishia huko mimi mshahara wangu hauzidi laki sita, nilifanyishwa vituko vyote ndani ya nyumba ,manyanyaso yote , hapiki hafui, hafanyi chochote ndoa ikawa inaelekea kuvunjika.

Nikaenda mahakamani kuprocess talaka wakasema mpaka nianzie baraza la usuluhishi la kata au kanisani, nikaamua kwenda kanisa tulilofungia ndoa tukaitwa kwa Baba Paroko for hearing sijui mediation sijui arbitration sijui mie nikatinga kwa bajaj ya kukodi nimepaukaaa yeye akaja na RAV4.

Baba Paroko alivyotusikiliza akaaniita pembeni akasema kijana hapa nadhani hata tukiomba na kukariri mistari yote ya biblia plus mapambio yote ndoa yako haitarudi kama mwanzo pambana utafute hela , huyu ni mchaga katumwa pesa mjini.

Nilisali sana nikasugua goti nikamuomba Mungu mara mambo yangu yakakaa sawa mshahara ukawa mara mbili plus marupurupu anagalau . baada ya miezi miwili sina hili wala lile mara simu yangu nilishangaa mke wangu kunipigia mchana , tumeachishwa kazi kmpuni imeuzwa, hureeeeee niliruka ruka kwa furaha sana nikapigia simu washikaji tukaenda kunywa bia na nyama choma mpaka saa sita usiku kabla polisi na makonda hawajatuvamia nilijua ile kazi ndio inaniharibia ndoa na aliipata kibahati hawezi tena kupata kazi kama ile.

Hela yote ya NSSF akajaribu kufanya kila biashara biashara zikabuma mtaji ukakata alijifanya hajui kupika sasa anapika kuliko hata wapishi wa Kempinski, alijifanya sijui hawezi kufua sasa anafua kuliko dobi, kitandani alijifanya mvivu sasa yuko vizuri kuliko wacheza shoo wa Fally ipupa , RAV4 imepaki tu muda wote ananilelea watoto kwa nini nisimshukuru Mungu
Funzo:
Mungu hujibu maombi ya wanaume haraka kuliko ya wanawake.

C&P from fb
 

Attachments

  • husband-wife.jpg
    13.1 KB · Views: 82
umeamua kurepeat again kova ongea tena vigodoro mwisho saa sita au tunakesha tena
 
Nimefurahi kusikia
"Nilisali sana nikasugua goti kumuomba Mungu"

Kuna faida kubwa katika hili, hasa ukiamini kwa 100%
Wengi tunashindwa kusubiria majibu na kukata tamaa.

Hongera sana.
 
Una bahati Ndg umemjua Mungu ukashuka kwake ukajibiwa!!
Mwingine angechukua hatua za hatari.
Ila kufanya sherehe ya kulewa mapombe hiyo hovyo kabisa.
Rudi kwa Mungu ushukuru kwa kuponya ndoa yako.
Mfanye muafaka na mkeo ili mtengeneze maisha mazuri ya ndoa yasiyo ma hila wala kukomoana!!
 
Dah nimecheka sana na hayo maneno ya mwisho.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah nimecheka sana na hayo maneno ya mwisho.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
😎
 
Ni muda muafaka sasa watanzania kujua historia yetu vizuri. Huyu mtema kuni ndio nani?
Kiswahili kimezaliwa kutokana na lugha mbalimbali kikiwemo kibantu.

Kutema kwa lughs za kibantu ni kukata.

'Kutema kuni' ama kifaa kinachotumika kukata kuni nadhani kinafahamika kwa ukali wake na madhara yake kikitumiwa 'kumtema' binadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…