Ze burner
JF-Expert Member
- Jan 5, 2011
- 514
- 83
Niliamua ku practice diet kama ilivyo kwetu wengi baada ya kusumbuliwa na kifriza kwa muda hivi. Aiseee! Nashuru sana ndani ya muda mchache nilipata matokeo chanya na hivi sasa nna kama nusu mwaka tena bado niko model. Tatizo kwa sasa nalazimika kubadili nguo zote kwa maana zote zimekuwa kubwa. Nimeamua kuacha diet ili kurudisha mwili kidogo walau niweze kuvaa baadhi tu ya nguo bado mwili umekataa kabisa kuongeza nyama. Sasa nimeongeza spidi ya kula kuliko mwanzo na bado empty. Naomba nifanyeje mana hadi za ndani zinapwerepweta sasa na kiukweli mimi haka kamwili hapana urudi tu uleule.