Nilifanya muziki nipate mademu - Dully Skyes

Nilifanya muziki nipate mademu - Dully Skyes

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Msanii Dully Skyes ambaye sasa anafanya vyema na ngoma yake 'Yono' amefunguka na kusema kuwa yeye alianza kufanya muziki wa bongo fleva ili awe mtu maarufu na kuanza kupata wanawake.
Dully%20Skyes.jpg

Msanii Dully Skyes

Dully Skyes alisema hayo leo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio kwenye Heshima ya bongo fleva na kusema miaka kumi na kitu iliyopita aliamua kuingia kwenye muziki na kuwa msanii ili apate wanawake.

"Mimi niliamua kuwa msanii ili kwanza niwe maarufu nipate mademu tu na kupendwa na wasichana kwa hiyo wala sikufikiri kuwa msanii ili nipate pesa ndiyo maana hata nilipolipwa elfu mbili kwa ajili ya show nilikubali japo nilitakiwa kulipwa elfu tano, tena hiyo elfu mbili niliona nyingi na nikamlipa Queen Darleen mia tano sababu nilikwenda naye kwenye show. Kwa hiyo sikuwahi kufikiria kama muziki ungekuwa biashara kama ilivyo sasa, saizi nafanya muziki biashara ikitokea hao wanawake wametokea ni 'by the way' tu" alisisitiza Dully Skyes

Dully Skyes ni moja kati ya wasanii ambao atakuwepo kwenye tamasha la 'Heshima ya bongo' fleva ambalo litafanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 1/7/2017 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala ambapo wasanii wengine kama TID, Dudubaya, Juma Nature, Z Anto, Solid Ground Family, Mabaga Fresh, Mandojo na Domokaya na wasanii wengine watawasha moto kwa ngoma zao kali za zamani.
 
Kwani hata wasanii wengine malengo yao huwa ni hayo hayo tu...
 
Bora maan muziki wa kitaa sn kipnd hicho zaid y kuwamendea totoz hakuna airtime wala nn
 
Hata Ss Sanaa Kwa Bongo Ni Kupata Umaarufu Na Kupata Mabwana Wenye Pesa Kwa Mabinti Na Kwa Wanaume Madem Wakali Km Ni Pesa Bac By The Way Tu.- By Hamorapa
 
Back
Top Bottom