SoC01 Nilifeli Darasani, nikafaulu Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Eng_Mwakibuti

Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
6
Reaction score
7
Habari, hi ni stori ya kweli inayo nihusu Mimi mwenyewe.

Nimeguswa kushea na wanajamii Forums, ili kuwatia moyo vijana na watu wengine ambao wanapambana kutoka kimaisha.

Kama Mtanzania wa kawaida nilizaliwa katika familia ya kipato cha chini sana. Nikiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita (kila mmoja na baba yake.) Tuliishi na mama yetu bila baba zetu.

Mama yetu hakuwa na kipato kikubwa, alijishughulisha na kazi ndogo ndogo za upishi (mama ntilie).

Tuliishi maisha ya kuhamahama maeneo mbalimbali Tanzania kutokea Mbeya, ambako Mimi kaka, Dada na mdogo wangu tulizaliwa mpaka Dar Es Salaam.

Mama yetu alioambana kutafuta pesa ilikutuhudumia watoto wake. Alitamani tusome na kuwa na kazi nzuri. Lakini hakuweza kutupeleka shule kutokana na Ada kuwa juu.

Hivyo aliamua kutupeleka shule mmoja mmoja kwa kuanza na kaka yetu mkubwa.

Hii ilipelekea sisi kuanza shule tukiwa wakubwa. Mimi nilianza darasa la kwanza nikiwa na miaka 11. Na hii ni baada ya Mh Rais B. Mkapa kufuta ada kwa elimu ya msingi mnamo mwaka 2000.

Haikuwa rahisi kwangu kusoma nikiwa na umri mkubwa, lakini nilimaliza elimu ya msingi na sikufanya vizuri.

Niliamua kurudi kitaa na kujishughurisha na kazi za upambaji wa kumbi na viwanja vya sherehe mbalimbali. Huku nikijisomesha kozi fupi fupi za kijasiliamali.

Mnamo mwaka 2011 niliamua kuitimiza ndoto ya mama yangu, kwa kurudi tena kusoma. Hivyo niliamua kujiunga na masomo ya QT, na nikafanya mtiani wa kidato cha nne 2012 nikaangukia division 4 kwa kupata D nne.

Niliamua kujiunga na chuo kusomea ufundi wa Computer 2014 katika chuo cha KIITEC. Lakini sikuchaguliwa, sikufanya vizuri mtiani wa kujiunga na chuo. Sikukata tamaa mwaka uliofuata mikarudi tena na KUFANYA mtiani wa kujiunga na chuo na nilichaguliwa.

Nilisoma kwa shida sana maana nilikuwa najisomesha mwenyewe. Chuoni tulikuwa tunaingia saa MBILI asubui tunatoka saa kumi na moja jioni. Kwa maana hiyo nilikuwa napata muda mfupi sana wa kutafuta pesa ya ada na ya kujikim.

Hiki kibanda kwa picha ndiko niliko anzia kazi za kupamba mwaka 2012.
2932116_inbound5269015487922724602.jpg

Nilikuwa napokea kazi za kupamba na ninapamba usiku kucha asubui naenda chuo jinoni naenda kutoa vitambaa ukumbini.

Kwa uweza wa Mungu nilifanikiwa kumaliza chuo salama mwaka 2018. Baada ya kumaliza chuo nilikuwa na matarajio ya kupata kazi, lakini haijawa hivyo. Nilizunguka mikoa mbalimbali Tanzania kutafuta kazi bila mafanikio.

Niliamua kutumia elimu niliyoipata kujiajiri. Nikafungua ofisi ya ufunfi Computer, umeme na simu. Haikuwa rahisi kupata wateja ila sikukata tamaa.

Kwa Sasa Mungu kanisaidia nimeweza kusimamia ofisi kwa Mika miwili na nusu na ofisi iko vizuri mpaka Sasa ninaweza kusaidia wengine kwa kuwapa nafasi ya kufanya kazi ofisini kwangu.

USHAULI WANGU

Nawasihi vijana wenzangu tusikate tamaa. Kikubwa tunapaswa kuwa na ndoto ya kufika mahali.
 
Upvote 4
Iyo kwenye picha ndo ofisi yako mkuu?
Happy ndipo nilipo anzia kabla sijaenda chuo. Hicho kibanda niyo ilikuwa mtaji wa kupamba.
Habari, hi ni stori ya kweli inayo nihusu Mimi mwenyewe.

Nimeguswa kushea na wanajamii Forums, ili kuwatia moyo vijana na watu wengine ambao wanapambana kutoka kimaisha.

Kama Mtanzania wa kawaida nilizaliwa katika familia ya kipato cha chini sana. Nikiwa mtoto wa tatu kati ya watoto sita (kila mmoja na baba yake.) Tuliishi na mama yetu bila baba zetu.

Mama yetu hakuwa na kipato kikubwa, alijishughulisha na kazi ndogo ndogo za upishi (mama ntilie).

Tuliishi maisha ya kuhamahama maeneo mbalimbali Tanzania kutokea Mbeya, ambako Mimi kaka, Dada na mdogo wangu tulizaliwa mpaka Dar Es Salaam.

Mama yetu alioambana kutafuta pesa ilikutuhudumia watoto wake. Alitamani tusome na kuwa na kazi nzuri. Lakini hakuweza kutupeleka shule kutokana na Ada kuwa juu.

Hivyo aliamua kutupeleka shule mmoja mmoja kwa kuanza na kaka yetu mkubwa.

Hii ilipelekea sisi kuanza shule tukiwa wakubwa. Mimi nilianza darasa la kwanza nikiwa na miaka 11. Na hii ni baada ya Mh Rais B. Mkapa kufuta ada kwa elimu ya msingi mnamo mwaka 2000.

Haikuwa rahisi kwangu kusoma nikiwa na umri mkubwa, lakini nilimaliza elimu ya msingi na sikufanya vizuri.

Niliamua kurudi kitaa na kujishughurisha na kazi za upambaji wa kumbi na viwanja vya sherehe mbalimbali. Huku nikijisomesha kozi fupi fupi za kijasiliamali.

Mnamo mwaka 2011 niliamua kuitimiza ndoto ya mama yangu, kwa kurudi tena kusoma. Hivyo niliamua kujiunga na masomo ya QT, na nikafanya mtiani wa kidato cha nne 2012 nikaangukia division 4 kwa kupata D nne.

Niliamua kujiunga na chuo kusomea ufunfi wa Computer 2014 katika chuo cha KIITEC. Lakini sikuchaguliwa, sikufanya vizuri mtiani wa kujiunga na chuo. Sikukata tamaa mwaka uliofuata mikarudi tena na KUFANYA mtiani wa kujiunga na chuo na nilichaguliwa.

Nilisoma kwa shida sana maana nilikuwa najisomesha mwenyewe. Chuoni tulikuwa tunaingia saa MBILI asubui tunatoka saa kumi na moja jioni. Kwa maana hiyo nilikuwa napata muda mfupi sana wa kutafuta pesa ya ada na ya kujikim.
2932116_inbound5269015487922724602.jpg

Nilikuwa napokea kazi za kupamba na ninapamba usiku kucha asubui naenda chuo jinoni naenda kutoa vitambaa ukumbini.

Kwa uweza wa Mungu nilifanikiwa kumaliza chuo salama mwaka 2018. Baada ya kumaliza chuo nilikuwa na matarajio ya kupata kazi, lakini haijawa hivyo. Nilizunguka mikoa mbalimbali Tanzania kutafuta kazi bila mafanikio.

Niliamua kutumia elimu niliyoipata kujiajiri. Nikafungua ofisi ya ufunfi Computer, umeme na simu. Haikuwa rahisi kupata wateja ila sikukata tamaa.

Kwa Sasa Mungu kanisaidia nimeweza kusimamia ofisi kwa Mika miwili na nusu na ofisi iko vizuri mpaka Sasa ninaweza kusaidia wengine kwa kuwapa nafasi ya kufanya kazi ofisini kwangu.

USHAULI WANGU

Nawasihi vijana wenzangu tusikate tamaa. Kikubwa tunapaswa kuwa na ndoto ya kufika mahali.

View attachment 1942636

Iyo kwenye picha ndo ofisi yako mkuu?

Engineer Mwakibuti, endeleea kupambana small progress ni mpango.
Asantee mkuu. Hicho kibanda ndiko niliko anziakazi now ninaofisi kubwa kuliko hicho kibanda
 
Back
Top Bottom