nilihama chumba lkn wapi

nilihama chumba lkn wapi

Joined
Jun 21, 2013
Posts
7
Reaction score
3
Jamani anayefahamu dawa au sumu inayomaliza kabisa mende aniambie hawa mifugo kwangu wamekua kero napuliza dawa lkn hawafi ndio sanazid kunenepa na kuzaliana kwa wingi.

DAWA IPI AU SUMU GANI NI BOMBA AU NITUMIE NN?
 
Kwanza USAFI hasa JIKONI. PILI tumia dawa hii NURVAN +AIKON changanya na puliza nyumba yote kwa ndani =mende utawasahau. ILA swala la usafi liendelee hata baada ya kupuliza hiyo dawa.
 
ilo tatizo si lako peke yako hata mie nasumbuliwa na hilo pia..
 
jamani anayefahamu dawa au sumu inayomaliza kabisa mende aniambie hawa mifugo kwangu wamekua kero napuliza dawa lkn hawafi ndio sanazid kunenepa na kuzaliana kwa wingi. DAWA IPI AU SUMU GANI NI BOMBA AU NITUMIE NN?

Acha uchafu, punguza makorokoro ndani, ipad wewe, iphone wewe, laptop wewe, nokia double line wewe, redio wewe, magazeti wewe, TV HDMI wewe king'amuzi wewe, redio kwenye gari wewe.
Huwezi kosa mende kamwe!
 
Tumia Rungu ila baada ya kupuliza chumba funga milango na madrisha at least for 3-4days then fungua na fagia na kupiga deki. Hakikisha mayai yao yote unayaharibu then zingatia usafi wa mara kwa mara. All the best.
 
hakikisha pia km kuna nyufa au vishimo unaviziba kwani ndio mazalia yao
 
Pole mkuu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tumia Rungu ila baada ya kupuliza chumba funga milango na madrisha at least for 3-4days then fungua na fagia na kupiga deki. Hakikisha mayai yao yote unayaharibu then zingatia usafi wa mara kwa mara. All the best.

3-4days???? Dawa yenyewe si inaishaga baada ya dakika 20 tu? Makusaro ndetengo andaa hela gesti kabisa uhamie ila ukirudi after 4days uje utupe majib manake ndo utakuwa umewapa mda wa kuzaliana bila bugudha
 
Hata usipotumia dawa USAFI ndo kila kitu
Hakikisha maliwato pako safi muda wote na uwe unasafisha kwa dawa na maji ya kutosha
Vyombo viwe safi na katka hali ya ukavu...tupa taka mbali na epuka mabaki ya vyakula mezani,jikoni kwenye fridge na kabatini na tumia dawa ikibidi
Mende wanaudhi sana
 
ilo tatizo si lako peke yako hata mie nasumbuliwa na hilo pia..

Mende hawakai nyumba ambao hakuna mabaki mabaki ya vyakula vinavyodondoka chini. Weka mazingira safi, utagundua hata bila kupiga dawa watasepa wenyewe.

Panya hakai geto la msela, hujui huu msemo?
 
Back
Top Bottom